Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Uzalishaji utajiri (mali) katika uchumi wa Kiislamu Chapa
05/10/2009

Uzalishaji mali katika Uislamu

Sharti la uongezaji utajiri wa taifa

Misingi ya kinadharia ya uchumi wa Kiislamu

Umuhimu wa uzalishaji na ugawanyaji wa utajiri

Uzalishaji utajiri(mali)

Uzalishaji mali bila kuzingatia uadilifu

Ugawanyaji wa utajiri

Vipimo vya ugawanyaji wa utajiri

Ugawanyaji wa utajiri katika mfumo wa Kiislamu

Mfuko wa Fedha wa Kimataifa

Uzalishaji utajiri (mali) katika uchumi wa Kiislamu

Uzalishaji mali katika Uislamu

Kuwa tajiri kwa kutumia njia halali na za kisheria hakuna tatizo lolote kwa mtazamo wa Uislamu. Viongozi wa serikali wanapaswa kuwafahamisha wananchi kuhusu njia za kuwashirikisha katika shughuli za kiuchumi. Sera hizi zina maana ya uzalishaji mali wa wananchi kwa ajili ya jamii. Uzalishaji mali hauna pingamizi kwa mtazamo wa Kiislamu. Uzalishaji mali ni tofauti na uporaji mali za watu wengine. Kuna wakati mtu hunyoosha mkono kuchota mali za umma; kuna wakati mtu hupata mafanikio ya kimaada bila ya kufuata sheria; kufanya hivyo ni marufuku; ama kwa kutumia njia za kisheria, kwa mtazamo wa sheria tukufu na kwa mtazamo wa Uislamu, uzalishaji mali ni jambo linalotakiwa na lenye kupongezwa. Zalisheni mali lakini isichanganyike na kufanya israfu. Uislamu unasema zalisheni mali lakini msifanye israfu. Tabia ya matumizi ya kupindukia haikubaliki katika Uislamu. Kile unachokipata kupitia uzalishaji mali, kitumie tena kama wenzo kwa ajili ya kuzalisha mali nyingine. Mali haitakiwi kulimbikizwa na kubaki bila kuzalishwa- ambayo katika Uislamu inajulikana kama ulimbikizaji mali- wala kutumiwa kwa fujo na israfu kwa mambo yasiyo na ulazima katika maisha; bali jizalishieni mali kwa kuzingatia mambo hayo. Mali wanazozalisha wananchi ni mali za nchi nzima; watu wote huwa wanafaidika nazo.

Juu ya ukurasa

Sharti la uongezaji utajiri wa taifa

Ili kuweza kuifanya nchi ijitosheleze na isiwe mhitaji kwa upande wa utajiri wa kitaifa, inapasa kuwepo fursa za uwekezaji wa vitega uchumi, harakati za kiuchumi na uzalishali mali kwa ajili ya wananchi wote walio amilifu; yaani inapasa watu wote wawe na uwezo wa kushiriki katika shughuli hizo. Serikali nayo inapaswa kutoa himaya na uungaji mkono kwa suala hilo; sheria nazo zinapaswa zitoe msukumo kwa suala hilo.

Juu ya ukurasa

Misingi ya kinadharia ya uchumi wa Kiislamu

Kuna misingi miwili mikuu katika uchumi wa Kiislamu. Njia yoyote ya kiuchumi, maelekezo au muongozo wowote wa kiuchumi ambao utaweza kutekeleza misingi miwili hiyo, unakubalika. Lakini muongozo wowote ule hata kama utategemea marejeo yanayoonekana kidhahiri kuwa ya kidini, kama utashindwa kutekeleza misingi miwili hiyo, hautokuwa wa Kiislamu. Mmoja kati ya misingi hiyo miwili ni “kuongeza utajiri wa taifa”. Nchi ya Kiislamu inapaswa kuwa nchi tajiri; haitakiwi kuwa nchi masikini; inatakiwa itumie utajiri wake na nguvu zake za kiuchumi ili kuweza kufanikisha malengo yake matukufu katika upeo wa kimataifa. Msingi wa pili ni “ugawanyaji wa kiadilifu wa utajiri na kuondoa hali ya unyonge ndani ya jamii ya Kiislamu”. Misingi miwili hii inapasa kutekelezwa. Na msingi wa kwanza ni sharti la kufikia kwenye msingi wa pili. Kama hakutakuwepo uzalishaji mali; kama pato la ziada la nchi halitoongezeka, haitowezekana kuondoa hali ya ufakiri na umasikini; kwa hivyo yote mawili yanahitajika.

Juu ya ukurasa

Umuhimu wa uzalishaji na ugawanyaji wa utajiri

Mambo mawili haya hayatakiwi kuchanganywa. Moja ni uzalishaji mali. Mtu ajishughulishe na harakati za kiuchumi kwa njia sahihi na kuzalisha mali. Na jengine ni namna ya uzalishaji na utumiaji wake. Sehemu ya kwanza ni ya jambo linalotakiwa kuwepo; kwa sababu mali yoyote inayozalishwa katika jamii, maana yake ni kwamba inaifanya majimui nzima ya jamii kuwa tajiri. Ama sehemu ya pili ambayo ni sehemu nyeti, ni kwamba uzalishaji utakuwa ni wa namna gani; isiwe ni wa njia zisizo za kisheria; isiwe ni wa kutumia hadaa na udanganyifu; na utumiaji wake usiwe ni wa namna isiyokubalika katika sheria ya dini; uweze kuwa ni mithili ya damu inayozunguka kwenye mishipa ya jamii; usiwe ni wa kutumika kwa mambo maovu.

Juu ya ukurasa

Uzalishaji utajiri(mali)

Uzalishaji unapasa kuwa nara ya taifa ya kuenezwa katika uwanja mpana. Uzalishaji kazi, uzalishaji elimu, uzalishaji teknolojia, uzalishaji mali, uzalishaji elimu ya fadhila tukufu, uzalishaji wa hadhi na izza, uzalishaji wa bidhaa na uzalishaji wa watu wenye uwezo na ufanisi; zote hizo ni aina za uzalishaji.

Mfumo wa Kiislamu unaiangalia kwa mtazamo chanya asili ya suala la uwekezaji, umuhimu wake na fikra ya uzalishaji mali kwa kutumia watu wenye mitaji wa ndani ya nchi, na unaliunga mkono kikamilifu suala hilo; na sababu ni kuwa jambo hilo linasaidia kuleta maendeleo, kukuza uchumi na kuandaa nafasi za ajira nchini. Chombo cha serikali ndicho kinachopaswa kuratibu sera zake kwa namna ambayo sambamba na uzalishaji mali- chambilecho baadhi ya jamaa, ulimbikizaji mali- kihakikishe kinadhamini pia uadilifu wa kijamii katika vitengo vyake vya uzalishaji. Ikiwa hautokuwepo ustawi wa kiuchumi katika jamii, ikiwa hautokuwepo uzalishaji wa kazi na uzalishaji wa mali, matabaka haya ya watu wanyonge na dhofulhali na hasa matabaka ya vibarua, ndio miongoni mwa watu watakaoumia na kuathirika zaidi. Na hivyo ndivyo adui anavyotaka iwe.

Viongozi ndio washika hatamu za masuala. Kwa upande mmoja inapasa waruhusu wale watu wanaofanya jitihada za kiuchumi kupitia njia sahihi na za kisheria- kwa sababu uchumaji mali hauchukuliwi na Uislamu kuwa ni jambo baya- lakini pia wasiruhusu utumiaji wa njia zisizo za kisheria, utumiaji wa njia za hadaa na udanganyifu, na utumiaji mbaya wa mali za umma; mambo hayo hayatakiwi.

Juu ya ukurasa

Uzalishaji mali bila kuzingatia uadilifu

Katika nchi tajiri zilizoendelea kiviwanda, si umasikini uliotokomezwa, si uadilifu uliojengwa wala si masuala ya maadili yaliyozingatiwa. Ijapokuwa uzalishaji mali umekithiri lakini kiwango cha maadili kimeshuka mpaka kufikia hali ya upotokaji. Katika ulimwengu wa kibepari, msingi mkuu wa kazi na harakati za kiuchumi ni uzalishaji mali tu. Katika mfumo huo msingi mkuu ni ukuaji wa uchumi, ustawi wa uchumi na uongezaji wa kiwango cha uzalishaji mali. Kila anayeweza kuzalisha na kuchuma mali zaidi na kwa ubora zaidi ndiye anayekuwa wa mbele. Tatizo huko si kutokea ubaguzi au tofauti ya kimatabaka. Tofauti katika kipato na hali ya watu wengi kukosa huduma za kijamii si jambo linaloushughulisha mfumo wa kibepari. Katika mfumo wa kibepari hata tadbiri zinazochukuliwa kwa ajili ya ugawanyaji wa utajiri, kwa mtazamo wa mfumo wa Ubepari ni tadbiri hasi na isiyokubalika. Mfumo wa Ubepari unaeleza kuwa:”hakuna maana yoyote ya kusema kuwa kusanyeni mali ili tuichukue kutoka mikononi mwenu na kuigawa! Hilo si jambo la maana. Ustawi hautopatikana kwa namna hiyo!”

Juu ya ukurasa

Ugawanyaji wa utajiri

Wale wanaosema kuwa uadilifu maana yake ni kugawana umasikini, kiini cha maneno yao ni kwamba msifatilie uadilifu; fuatilieni uzalishaji mali ili mali kiwe ndiyo kitu kinachogawanywa. Kufatilia uzalishaji mali pasina kuzingatia uadilifu ndicho kitu kinachoshuhudiwa leo hii katika nchi za Kibepari. Katika nchi iliyo tajiri zaidi duniani- yaani Marekani- kuna watu wanaofariki kutokana na njaa, baridi kali na joto kali; hiyo ni hali halisi inayoshuhudiwa huko.

Kitu ambacho kina umuhimu wa kwanza kwa mfumo wa utawala wa Kiislamu ni kuhakikisha ndani ya nchi, watu wote wanafaidika na neema zilizopo; kusiwepo umasikini; kusiwepo ubaguzi; kusiwepo utumiaji usio na usawa wa fursa na suhula; na kusiwepo utumiaji wa sheria usio na usawa.

Juu ya ukurasa

Vipimo vya ugawanyaji wa utajiri

Wakati suala la uzalishaji mali linapotenganishwa na mtazamo wa msingi wa uadilifu, hali katika jamii hufikia hadi, wale watu walio mahodari na wajanja zaidi huweza kwa usiku mmoja tu kujipatia mali na utajiri mkubwa; kwa hivyo kusema kwamba msizungumzie uadilifu, zungumzieni uzalishaji mali; na kisha kuleta kisingizio pia kwamba ni baada ya uzalishaji mali ndipo tutafuatilia suala la uadilifu, hilo halikubaliki. Uadilifu maana yake ni kuhakikisha kuwa suhula zilizopo nchini, zinagawanywa kiadilifu na kimantiki- na si kiadilifu bila mipango maalumu- na kujaribu kuhakikisha kuwa suhula hizo zinaongezeka zaidi ili ziweze kuwafikia kwa wingi zaidi watu wote.

Juu ya ukurasa

Ugawanyaji wa utajiri katika mfumo wa Kiislamu

Mfumo wa Kiislamu unaitakidi juu ya kuwa na jamii tajiri, na si jamii masikini na iliyobaki nyuma kimaendeleo. Unaitakidi juu ya suala la ustawi wa kiuchumi; kinachopewa kipaumbele cha kwanza ni kuhakikisha hakuna masikini katika jamii; hakuna mtu mnyonge; hakuna ubaguzi katika utumiaji wa suhula za umma. Kila mtu ambaye ameweza kujiandalia suhula yeye mwenyewe, suhula hizo ni mali yake mwenyewe. Ama zile ambazo ni mali ya umma kama vile fursa na suhula, hiyo ni mali ya nchi nzima na lazima ihakikishwe hakuna ubaguzi katika kufaidika na vitu hivyo. Isidhaniwe kwamba lengo la mfumo wa Kiislamu ni kuongeza kiwango cha utajiri wa kimaada! Yaani baadhi ya watu waweze kuwa na anuai na njia mbali mbali za uzalishaji mali; wastani wa pato la kila mtu nchini liongezeke maradufu kutoka kiwango fulani hadi kiwango fulani, au pato lote la uzalishaji wa nchi liongezeke kutoka kiwango fulani hadi kiwango fulani. Bila shaka vipimo hivi vinaweza katika baadhi ya hali kuwa vielelezo vya kupiga hatua kuelekea kwenye uadilifu; lakini si mara zote inakuwa hivyo.

Juu ya ukurasa

Mfuko wa Fedha wa Kimataifa

Wale watu walioko kwenye sehemu kuu za uratibu wa mipango au vituo vya kielimu na utafiti, wanaobuni fikra na kuandaa mipango kuhusu uchumi, kuhusu siasa, kuhusu siasa za kimataifa na kuhusu masuala muhimu ya nchi nyingine wasitumie fomyula za Magharibi; fomyula za kiuchumi za Magharibi, fomyula za Benki ya Dunia au Mfuko wa Fedha wa Kimataifa na kuzioanisha na masuala ya nchi yetu; si sawa kufanya hivyo; nadharia hizo hazifai kwa nchi ya Iran. Bila shaka elimu yao itatumiwa. Popote pale penye maendeleo ya kielimu, penye tajiriba na uzoefu wa kielimu, tutafaidika napo; lakini mipango inayoratibiwa ilingane na fikra na mahitaji ya taifa.

Mahathir Muhammad, Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia- ambaye alikuwa mtu mchapakazi sana, makini na asiye na mzaha- alikuja hapa Tehran, na akaja kuonana na mimi pia; na ilikuwa ni wakati ule yalipokuwa yamejiri matukio mbali mbali katika Asia ya Mashariki huko Malaysia, Indonesia na Thailand, na ulipokuwa umetokea mtikisiko mkubwa wa kiuchumi. Alikuwa ni bepari huyu wa kizayuni, na baada ya yeye wakafuatia mabepari wengine, ambao kwa kutumia hila na mbinu za kibenki na kifedha waliweza kuzifilisisha nchi kadhaa. Wakati ule Mahathir Muhammad aliniambia: kitu pekee ninachoweza kukueleza ni kwamba baada ya usiku mmoja tu tumekuwa ombaomba! Bila shaka ndivyo inavyokuwa wakati nchi inapokuwa na utegemezi wa kiuchumi, na ikataka kutekeleza maelekezo ya kiuchumi ya Benki ya Dunia na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa. Hii Benki ya Dunia yenyewe na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa, nazo pia ni sehemu mojawapo ya kitendawili hiki kikubwa.

Hili ni jambo la hatari sana kwamba hatamu za masuala ya ulimwengu kuwa mikononi mwa magenge ya madola yenye nguvu duniani; ambavyo ndivyo ilivyo hii leo.

Juu ya ukurasa

 
< Nyuma   Mbele >

^