Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Vijana kwa mtazamo wa Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei Chapa
21/04/2010

Umuhimu wa Ujana

Umuhimu wa Kipindi cha Ujana
Uislamu Unakipa Umuhimu Mkubwa Kipindi cha Ujana
Rasilimali ya Maendeleo ya Mataifa
Sifa Maalumu za Vijana Zinazostahiki Kupongezwa
Vijana na Jukumu la Viongozi

Majukumu ya Kijamii ya Vijana

Kujijenga Kinafsi katika Vipengee Vyote
Hisia za Kubeba Majukumu Kimwamko
Hisia Kali za Vijana Kuhusu Masuala ya Kijamii
Juhudi kwa ajili ya Kufikiri na Kutilia Maanani Mambo

Vizuizi na Changamoto za Kizazi cha Vijana

Wasiwasi Alio Nao Kijana
Wasiwasi wa Kimaanawi
Haja ya Kugundua Utambulisho na Kipaji
Kuamiliana Kihoja na Kijana
Hisia za Kijinsia
Mashambulizi ya Kiutamaduni
Uvivu na Kupenda Wepesi na Starehe
Kuvunjika Moyo
Madhara Yanayowakabili Vijana wa Kiislamu
Kupambana na Madhambi

Siri ya Maendeleo ya Vijana

Hazina Isiyoisha
Kutawakali kwa Mwenyezi Mungu
Kutia Nguvu Moyo wa Kujiamini
Juhudi za Kielimu
Kutumia Vizuri Wakati

Maswali ya Vijana na Majibu ya Ayatullah Khamenei

Vigezo vyako katika kipindi cha ujana wako walikuwa ni watu gani?
Umepitisha vipi kipindi chako cha ujana?
Vitu gani vya kuburudisha vilikuwa vikijaza wakati wako katika kipindi cha ujana wako?
Kwa mtazamo wako, kijana wa Kiislamu anapaswa kuwa na sifa gani? Vipi kijana anaweza kupitisha kipindi cha maisha yake na akafanikiwa kufikia malengo yake?
Kijana anaweza vipi kudhibiti hisia zake za kupenda mambo ya kusisimua na anaweza kufaidika nazo vipi hisia hizo?
Unapowaona vijana unakuwa na hisia gani na neno la kwanza unalopenda kuwaambia ni kitu gani?
Unawapa miongozo gani vijana ya kuweza kuitumia katika maamuzi yao mbali mbali ya kijamii na kisiasa?
Je, uko uwezekano wa kujazwa pengo lililopo baina ya Iran na nchi zilizoendelea?

Vijana kwa mtazamo wa Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei

Umuhimu wa Ujana

Umuhimu wa Kipindi cha Ujana

Ujana ni kitu kizuri mno na ni kipindi kisicho na mfano wake na kisichomithilika na chochote katika maisha ya mwanaadamu. Nchi yoyote ambayo italipa umuhimu wake suala la vijana vile linavyostahiki, basi bila ya shaka yoyote nchi hiyo itapata maendeleo na mafanikio makubwa sana. Ujana yaani kile kipindi cha mg’aro na mmeremeto katika maisha ni kipindi ambacho ijapokuwa si kirefu, lakini athari zake ni kubwa mno na ni za muda mrefu sana katika kipindi kizima cha maisha.

Kama ambavyo macho ya vijana yana nishati, nguvu na damu changa, nyoyo zao nazo zimejaa nishati. Mwenyezi Mungu amemuumba kiumbe huyu akiwa na nguvu zote hizi za kufikiri, nguvu zote hizi za kiakili, uwezo wake wote huu wa kimwili, nguvu zake zote hizi za kihisia na mbinde nyinginezo nyingi zisizojulikana ili aweze kutumia maumbile yake hayo na mazingira anayoishi kama njia bora kabisa ya kuweza kujikurubisha kwa Muumba wake.

Juu ya ukurasa

Uislamu Unakipa Umuhimu Mkubwa Kipindi cha Ujana

Bwana Mtume Muhammad SAW ametuusia kuhusu vijana akisema inabidi tuwape umuhimu mkubwa vijana na tutumie nguvu za vijana kwa ajili ya kufanya kazi kubwa kubwa. Amirul Muuminin Ali bin Abi Talib AS katika kipindi chake cha ujana wakati alipokuweko Makkah alikuwa ni kijana mwenye kujitolea, kijana mwenye akili kubwa na kijana mwanaharakati ambaye daima alikuweko katika mstari wa mbele wa kutekeleza mambo mema. Alikuwa akiondoa vizuizi mbali mbali vikubwa vilivyokuwa vikijitokeza katika njia ya Uislamu na katika kazi za Bwana Mtume. Alikuwa wa kwanza kujitokeza katika medani za hatari na alichukua jukumu la kutekeleza kazi nzito zaidi. Alikuwa tayari kutoa roho yake wakati Bwana Mtume alipoamrishwa na Mwenyezi Mungu ahamie Madina. Huko mjini Madina pia, alikuwa kamanda wa jeshi, alikuwa kamanda wa vikosi amilifu, alikuwa msomi, mwenye busara na akili nyingi na alikuwa mungwana na mwepesi wa kusamehe. Katika medani ya vita alikuwa ni mwanajeshi shujaa na kamanda wa mstari wa mbele. Katika upande wa utawala na siasa alikuwa ni mtu muhimu na mwenye uwezo mkubwa. Katika uga wa masuala ya kijamii pia alikuwa ni kijana aliyeendelea kwa maana halisi ya neno. Katika kipindi cha miaka 10 ya serikali yake, Bwana Mtume Muhammad si tu alitumia kadiri alivyoweza kipaji cha mtu kijana kama Imam Ali, bali pia alitumia vilivyo vipaji vya vijana wengine wa zama hizo kwa kadiri ilivyomyumkinikia.

Juu ya ukurasa

Rasilimali ya Maendeleo ya Mataifa

Tunapoiangalia idadi ya vijana na kuilinganisha na jamii nzima ya wananchi wa Iran tutaona kuwa, vijana wanaunda jamii ya ajabu nchini Iran. Leo hii zaidi ya nusu ya wananchi wa Iran ni watu ambao wana umri wa chini ya miaka 30. Tukio la aina yake lililotokea hapo ni kwamba nchi ya Iran ambayo ni yenye idadi kubwa zaidi ya vijana kulingana na idadi ya wananchi wake, imeshuhudia mapinduzi makubwa zaidi katika historia, mapinduzi ya vijana zaidi kuliko mapinduzi yote mengine duniani na mfumo ulio huru kabisa wa kisiasa kuliko sehemu yoyote duniani. Mlingano huo kwa kweli ni mlingano wa ajabu sana. Idadi hiyo kubwa ya vijana haiishi katika nchi ambayo mfumo wake wa kisiasa ni kibaraka wa Marekani na makampuni makubwa ya kifedha duniani wala mashirika yanayomilikiwa na mataifa kadhaa na wala si nchi inayofuata nchi nyingine au mfumo wa nchi fulani wa kisiasa. Bali wanaishi katika nchi ambayo mfumo wake wa kisiasa unakubalika mbele ya vijana. Vijana wanahitaji kuwa huru. Kiasili tabia ya vijana ni kutaka kuwa huru na hawapendi kuinamisha tu vichwa vyao na kufuata kibubusa mambo. Mfumo wa leo wa kisiasa nchini Iran ni mfumo ambao unampa fakhari kijana na kumfanya asiwe dhalili mbele ya mtu yeyote na licha ya kuweko vitisho na mashinikizo mengi ya Marekani katika kipindi chote hiki, lakini kijana wa Kiirani kamwe hajawahi kuogopeshwa na vitisho hivyo hata mara moja. Nchi ya Iran inaendelea kupata uzoefu wa mapinduzi mapya na ya vijana. Hivyo Iran inahitaji kuwa na kasi katika kazi zake sambamba na mipangilio sahihi kwa ajili ya kujijenga na kujiendeleza kadiri inavyowezekana ili kwa njia hiyo taifa hili liweze kukata ulimi wa adui na kutia nguvu uwepo wake katika nyanja zote, ziwe za kielimu au za kimatendo. Jamii ambayo nusu ya watu wake ni vijana inapoingia kwa kasi katika medani huifanya jamii hiyo ifanikiwe katika mambo yake na mustakbali wake huwa bora kikamilifu.

Juu ya ukurasa

Sifa Maalumu za Vijana Zinazostahiki Kupongezwa

Kwa kwa kawaida kijana huikubali haraka haki. Jambo hilo ni muhimu sana. Kwa kawaida kijana hupinga na kulalamikia jambo kiukweli na kiudhati wa moyo na hufanya mambo yake bila wasiwasi wala mashinikizo yoyote ya ndani. Jambo hilo nalo ni muhimu sana. Kukubali kirahisi, kupinga na kukataa jambo kwa udhati wa moyo na kuchukua hatua bila wasiwas. Zikusanyeni pamoja sifa zenu hizo. Mkifanya hivyo mtaona wenyewe ni uhakika bora kiasi gani utazaliwa hapo na mtaona wenyewe ni kiasi gani jambo hilo linaweza kutatua matatizo yote yanayojitokeza.

Kimaumbile kijana ni mtu anayependa mageuzi. Dhati ya kijana (wa Kiislamu) ni kupenda uadilifu, uhuru unaokubalika kisheria na kufanikisha malengo matukufu ya Kiislamu. Uhakika na malengo matukufu ya Kiislamu humtia hamasa kijana na kumpa mvuto mkubwa. Wakati anapokumbuka sifa ya kipekee aliyokuwa nayo kijana kama Amirul Muminin Ali AS, humsisimua kijana huyo na kumfanya alinganishe mapungufu yaliyopo na hali yake na baadaye kutaka mageuzi na mabadiliko. Sifa hiyo ni nzuri sana.

Miongoni mwa sifa zinazostahiki kusifiwa na kupongezwa za ujana, nguvu na uwezo, ni ubunifu na nishati anayokuwa nayo kijana. Je kijana ameshaitumia vizuri fursa hiyo? Hapana. Bado vijana hawajafanya juhudi zinazotakiwa kwa ajili ya kutumia vizuri fursa ya kupigania haki, nguvu, nishati, kutokimwa na kutochoka sambamba na hima yake ya ujana. Hiyo ni hatua ya kimaumbile katika umri na maisha ya kila mtu. Hivyo hiyo ni tunzo muhimu na kuna majukumu ambayo kijana anapaswa kuyatekeleza katika mkabala wa tunzo hiyo.

Juu ya ukurasa

Vijana na Jukumu la Viongozi

Kazi ya kulea vijana si jukumu la wazazi wawili tu, bali maafisa wa elimu, wakuu wa kisiasa na wapangiliaji wa mipango ya kiuchumi nchini, wote hao wanahesabiwa kuwa ni sehemu ya watu wenye jukumu la kulea vijana katika jamii. Vijana nchini ni watoto wa viongozi wa nchi. Kama utapata nguvu uhusiano wa baba na mwana kati ya viongozi na tabaka la vijana, basi matatizo mengi yataweza kutatuliwa. Baadhi ya matatizo hayo yanaweza kutatuliwa katika kipindi cha muda mfupi na mengine lakini huenda yasitatuke katika kipindi hicho kifupi. Sasa lililo muhimu ni kuelimishwa vijana na hata kutumia ushauri na msaada wao ili kutatua matatizo hayo na kuondoa mapungufu yanayojitokeza.

Idadi kubwa ya vijana nchini Iran ni sawa na mto wenye mawimbi makali. Maji ya mtu huo yanataririka mtawalia bila kusita na yataendelea hivyo kwa miaka mingi baadaye. Kuna njia mbili za kuamiliana na mto huo:

Muamala wa kwanza ni kuwa, kabla ya jambo lolote, viongozi wanapaswa kutumia akili, busara na njia za kielimu kutambua umuhimu wa mto huo. Pili ni kutambua ni sehemu gani inabidi maji ya mtu huo yatiririke. Tatu waweke mipango mizuri na kufungulia njia maji ya mto huo ili yaelekee kule kunakotakikana. Ni wakati huo ndipo maelfu ya konde, mashamba na mabustani yataweza kufaidika na kunawirishwa na neema hiyo isiyo na mwisho na kupelekea kila sehemu iliyoharibika iweze kutengenea na kuneemeka. Aidha inawezekana kuuelekeza mto huo wenye mawimbi makali upande wa mabwawa ya kuzalisha nishati na kuufanya kuwa chanzo cha nishati na nguvu kubwa za kuifanya nchi nzima iwe amilifu na ipate msukumo wa kufanya juhudi kubwa zaidi. Kama maudhui hiyo itaamiliwa namna hiyo, basi vijana watakuwa ni kizazi chenye baraka nyingi zisizo na kifani na watakuwa ni kizazi cha aina yake kiasi kwamba hata kama watu wote, kila mmoja wao atakaa na kumshukuru Mwenyezi Mungu mara mia kila siku, bado itakuwa Mwenyezi Mungu hajashukuruwia vile inavyotakiwa. Njia bora ya kuweza kulifanya jambo hilo lifanikiwe, ni kuwa na mipangilio mizuri, ni kuongoza vyema, ni kufungua njia, ni kuainisha nukta inayotakiwa ili kwa njia hiyo iwezekane kuiongoza kwenye nukta hasa inayotakiwa. Matunda ya kuweko neema hiyo yenye thamani kubwa na atia hiyo ya Mwenyezi Mungu; ni kunawiri, kuneemeka, kustawi, na kuongezeka nishati na baraka za Mwenyezi Mungu.

Muamala mwingine ni viongozi kuuacha kama ulivyo mto huo wenye mawimbi makali, wasifikirie njia za kuuongoza na wasiuwekee mipango yoyote na wasijue thamani yake. Wakifanya hivyo bila ya shaka matokeo yake yatakuwa si tu kukauka mashamba na kuangamia mabustani, bali hata maji ya mto huo nayo yatapotea bure. Kwa uchache maji hayo yataelekea baharini na kuchanganyika na maji ya chumvi na kupotelea huko. Lakini matokeo yake mengine ni kukusanyika maji ya mto huo katika maeneo yaliyojaa maradhi au kujazana mahali pamoja yakitafuta njia ya kutokea. Matokeo yake ni kuzuka mafuriko na kuangamiza matunda ya mashamba ya watu. Kama kutakosekana mipangilio mizuri na iwapo hakutafanyika kazi zenye umakini, bila ya shaka matunda hayatakuwa kitu kingine ghairi ya hayo tuliyotangulia kusema.

Juu ya ukurasa

Majukumu ya Kijamii ya Vijana

Kujijenga Kinafsi katika Vipengee Vyote

Kujiimarisha kielimu na kujijenga kimaadili na kimwili ni mambo ambayo kila kijana anapaswa kuwa nayo na kwa kweli kijana anahitajia mambo kama hayo. Kijana anapaswa kuwa na maamuzi katika uwanja wake na anapaswa apande mbegu yake na atumie vizuri hazina na utajiri wake wa kiutamaduni. Athamini azma na irada yake kwa ajili ya kujenga shakhsia na uhuru wake. Asikubali kufuata kibubusa tu mambo au kuwafanya watu wasio na maana kuwa kigezo chake.

Vijana wasikae na kusubiri kufuata tu mambo. Bali wanapaswa kufikiria mbinu na njia mbali mbali ambazo ndani yake wataweza kuimarisha na kutia nguvu akili, irada na imani zao na kuyafanya maadili na akhlaki zao kuwa safi na nyoofu. Kama atafanya hivyo basi kijana atakuwa ni kiungo muhimu ambacho kitakuwa mithili ya nguzo madhubuti na dari isiyotetereka ya nchi hii na atakuwa ni kama chombo makini ambacho ustaarabu wa kweli wa taifa hili unaweza kuingia na kuimarika ndani yake.

Juu ya ukurasa

Hisia za Kubeba Majukumu Kimwamko

Jambo ambalo ni muhimu kwa vijana ni kuwa na mwamko wa kubeba majukumu. Kijana ni mtu aliyejaa nishati na nguvu na hisia zake ni kali zaidi. Maana ya kuwa na hisia za kubeba majukumu ni kwamba, kama ambavyo mtu anahisi kuwa ni wajibu wake kubeba jukumu la maisha yake, kazi zake, ndoa na kila kitu kinachomuhusu yeye binafsi, ahisi wajibu pia wa kubeba jukumu kuhusu malengo yaliyo juu zaidi, aone ana wajibu wa kufanikisha malengo ambayo hayamuhusu yeye tu bali yanalihusu taifa zima, historia nzima na ubinaadamu wote kiujumla. Mwanaadamu anapaswa kuhisi wajibu wa kubeba jukumu la kufanikisha malengo hayo na achukue dhima, masuuliya na kafala ya kufanikisha muradi na maarubu hayo. Hakuna mwanaadamu wala jamii yoyote itakayoweza kufikia vilele vya juu vya ujazi, uneemevu na fanaka bila ya kuwa na hisia za wajibu wa kubeba majukumu ya kufanikisha shabaha zake. Hisia hizo nazo za kuhisi kila mtu ana wajibu wa kubeba majukumu zinapaswa ziwe za kimwamko. Kila mtu anapaswa ajue anachokusudia kufanya na ajue namna ya kukabiliana na vizuizi vyovyote katika juhudi za kufanikisha malengo yake. Jambo hilo ndilo linaloitwa kuhisi wajibu wa kubeba majukumu kimwamko.

Juu ya ukurasa

Hisia Kali za Vijana Kuhusu Masuala ya Kijamii

Kwa kawaida kijana huguswa na huwa na hisia kali kuhusu masuala ya kijamii. Kama katika jamii - yaani hali na mazingira yote anayokuwemo ndani yake kijana – kutakuwa na ubaguzi wa aina yoyote ile, basi hali hiyo humuudhi kijana. Kama ndani ya familia kutakuwa na ubaguzi, jambo hilo humkasirisha kijana, kama shuleni na darasani kutakuwa na ubaguzi, upendeleaji huo hutonesha hisia za kijana. Kuna baadhi ya watu wamepoteza nguvu za kuguswa na matatizo hayo ya kijamii au wanaguswa tu na maisha yao binafsi au wameona sana mambo hayo kiasi kwamba imekuwa ni jambo la kawaida kwao, lakini hali haiko hivyo kwa kijana. Kijana ni mtu anayependa kuona kila kitu kinakwenda sawa na kiko mahala pake. Kama utakosekana uadilifu katika jamii, kama kutakuwa na ubaguzi na upendeleo, hali hiyo humuudhi kijana. Kama jamii itatawaliwa na ufisadi, bila ya shaka yoyote hali hiyo haiwezi kuvumiliwa na kijana anayetaka kuona nchi yake inaendelea na kuwa na heshima. Wakati jamii inapokuwa imejaa hamasa na mwamko wa kitaifa, utamuona kijana amechachamaa na yuko mstari wa mbele katika masuala mbali mbali yanayohusu jamii hiyo. Wakati wa vita vya kulazimishwa vilivyoanzishwa na Iraq dhidi ya Iran, Imam Khomeini (quddisa sirruh) alitoa ishara tu na vijana wakajitokeza makundi kwa makundi na kwenda vitani licha ya kwamba vijana hao walikuwa na yakini kwamba huko wanakokwenda kuna hatari kubwa. Ingawa hivyo ndivyo walivyo vijana katika jamii zote, lakini katika jamii ambazo zimejipambanua kiimani, jamii ambayo inayapa umuhimu mkubwa matukufu ya kimaanawi, hali hiyo inashuhudiwa zaidi. Wakati linapofika suala la kuilinda nchi katika jamii yoyote ile, au linapofika suala la kulinda heshima na matukufu ya taifa na uhuru na amani ya nchi, utaona vijana wa jamii hiyo wako mstari wa mbele kujitolea katika medani za hatari na kuchukua hatua mbali mbali bila ya kuwa na wasiwasi wowote wa kimaisha au woga wa kupoteza starehe zao.

Juu ya ukurasa

Juhudi kwa ajili ya Kufikiri na Kutilia Maanani Mambo

Miongoni mwa mambo ya lazima anayopaswa kuwa nayo kijana mwanamapambano ni kujipinda katika kutafuta elimu, kupambana na uvivu, kupambana na fikra za kupenda starehe zaidi kuliko kujali masuala ya masomo, bali inabidi kijana ajibidiishe katika kufikiria mambo ya maendeleo. Basi inabidi kijana ajizoeshe kufikiria masuala muhimu ya kimaendeleo kwani kufanya hivyo nako ni mapambano. Moja ya hatari kubwa zinazomkabili kila mtu na hasa vijana ni kwamba pale anapokumbwa na matukio mbali mbali katika jamii anashindwa kuwa na fikra za kuyatatua au kupambanua baina ya zuri na baya. Kwa kweli jukumu la kumwongoza kijana ni kazi nzito na ngumu na tab’an watu mbali mbali wana wajibu wa kuwaongoza vijana katika njia sahihi, lakini vijana wenyewe nao wana jukumu la kuwa na fikra pana zitakazowafungulia njia ya kutatua masuala yao. Vijana wanapaswa kujizoesha kutatua mambo yao wenyewe yawe makubwa au madogo. Wajipinde katika masuala ya kusoma na kutalii mambo mbali mbali na wasichoke kustafidi na ushauri wa watu wengine. Miongoni mwa mambo ambayo yanamkosesha mtu fursa ya kufikiria masuala muhimu ni kughariki na kuzama katika ufisadi na kukosa matumaini. Hivyo moja ya majukumu makubwa ya vijana ni kupambana na masuala ya ufisadi, kuvunjika moyo haraka na kutokuwa na matumiani.

Juu ya ukurasa

Vizuizi na Changamoto za Kizazi cha Vijana

Wasiwasi Alio Nao Kijana

Jambo la kwanza kabisa linalomtia wasiwasi kijana na kuishughulisha akili yake ni elimu, kazi na mustakbali wa maisha yake. Kwake yeye ni jambo muhimu sana kudhamini mustakbali wake na kujua vyema anaelekea wapi. Akili ya kijana hushughulishwa sana na masuala ya kuwa na mke au kuwa na mume na kuwa na familia, hushughulishwa sana na masuala ya kutafuta elimu na kuwa na nafasi muhimu katika jamii, ni muhimu kwake kuwa na vitu vya kumsisimua na kumchangamsha na mambo hayo ni miongoni mwa sifa maalumu nzuri alizo nazo mwanaadamu. Mambo hayo yanashuhudiwa kwa uwazi zaidi kati ya vijana na ni vitu vinavyohusiana na hisia za dhati ya mwanaadamu. Mambo kama haya ni muhimu sana kwa vijana. Hata hivyo hayo sio mambo pekee yanayoshughulisha fikra za vijana.

Juu ya ukurasa

Wasiwasi wa Kimaanawi

Miongoni mwa wasiwasi na mambo yanayoishughulisha fikra ya kijana ni suala la umaanawi. Hiki ndicho kitu ambacho inabidi watu wakae na kukifanyia kazi. Kwa kawaida katika kipindi fulani cha ujana hushudiwa kwa uwazi zaidi roho ya kimaanawi na kidini. Kijana katika kipindi hicho hutamani wakati wote awe karibu na Mwenyezi Mungu. Anapenda awe na mawasiliano na kituo kikuu cha umaanawi na kambi adhimu ya uhakika na umaanawi. Ndio maana utaona vijana wengi wakishiriki katika jalsa na majlisi za kimaanawi na kama katika mazingira hayo, dini ya jamii hiyo haitaonyesha utepetevu, basi faida za kushiriki vijana katika maeneo kama hayo huwa ni kubwa sana. Hata hivyo na ingawa hayo ndiyo maumbile ya mwanaadamu ya kuhisi kuwa hajakamilika anapokosa masuala ya kimaanawi, lakini dini nyingi duniani katika nchi tofauti ulimwengu unazipata zinashindwa kuwa na ile roho na umaanawi unaotakiwa wa kuweza kuwaathiri vijana. Ndipo unaona vijana wengi wa nchi hizo wanakuwa mbali na masuala ya kidini na kimaanawi. Lakini katika jamii ambayo suala la dini na umaanawi linapewa haki yake na linadhihirishwa kwa maana yake halisi, vijana katika jamii hizo utawaona wanapenda sana dini na hujitokeza kwa wingi sana katika masuala yanayohusiana na umaanawi na mafundisho ya dini yao.

Kwa hakika ibada inakosha na kusafisha nyoyo na roho za wanaadamu. Ibada ni johari yenye thamani kubwa na kima cha hali ya juu. Hivyo wale watu ambao vipaji vya nyuso zao havimsujudii Mwenyezi Mungu Ambaye Ndiye Haki na Uhakika wa kweli, basi wanajinyima wenyewe neema kubwa sana na kamwe hawawezi kuidiriki ile ladha na utamu hasa wa kimaanawi. Kuwa na mfungamano wa karibu na Mwenyezi Mungu, kuomba sana dua na kunong’ona na Mola Muumba, kutaradhia na kumlilia hali Mwenyezi Mungu katika mambo yote, Mola Ambaye Ndiye Mkwasi na Tajiri Mutlaki, kuomba msaada wa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kufikia malengo matakatifu, yote hayo anaweza kuyapata mwanaadamu kupitia ibada. Uchaji Mungu bora kabisa hupatikana katika ujana. Ibada ya kijana huwa na thamani kubwa zaidi, huwa bora zaidi, huvutia zaidi, huwa na umaanawi mkubwa zaidi na dua ya kijana huwa rahisi sana kutakabaliwa na Mwenyezi Mungu.

Juu ya ukurasa

Haja ya Kugundua Utambulisho na Kipaji

Mtu katika kipindi chake cha ujana hususan katika ule wakati wa mwanzoni kabisa mwa ujana wake, huwa ana matumaini ya kufanikiwa katika vitu vingi na mambo mengi yanamsukuma kufanya vitu tofauti. Mosi na kutokana na kuwa wakati huo huwa yuko katika hali ya kuundika utambulisho wake mpya, kijana hupenda shakhsia yake hiyo mpya itambuliwe na iheshimiwe na wote ambapo mara nyingi hali haiwi hivyo kwani aghlabu ya wakati hushuhudiwa baba na mama wakishindwa kuitambua rasmi na shakhsia yake hiyo na huwa hawalipi nguvu suala hilo. Pili ni kwamba kijana anakuwa na hisia na misukumo yake maalumu. Wakati huo mwili wake huzidi kukuwa na roho yake pia, na huwa yumo katika kuingia kwenye ulimwengu mpya ambapo mara nyingi utapata watu wanaomzunguka, familia yake na watu katika jamii wanashindwa kuudiriki na kuuelewa ulimwengu wake huo mpya. Baadhi ya wakati wanafanya makusudi kutoujali ulimwengu wake huo hivyo kijana anajihisi kuwa pweke na kujiona anaishi katika jamii ambayo watu hawamwelewi kabisa. Hebu watu wazima na wakae na kufikiria kipindi chao cha ujana. Mtu katika kipindi chake cha ujana, iwe ni mwanzoni mwa kubaleghe kwake au baada yake hukabiliwa na vitu vingi vilivyo vigeni kwake. Ndani ya akili yake hujaa udadisi na mambo mengi asiyoyajua na ambayo anatamani apate mtu amfafanulie lakini mara nyingi hukosa majibu ya haraka au ya kukinaisha na hapo kijana huhisi amepungukiwa na vitu vingi. Nne ni kwamba kijana huhisi kuwa ana nguvu nyingi za kumwezesha kufanya lolote lile iwe ni kwa kutumia nguvu zake za kimwili au nguvu zake za kifikra na kiakili. Ukweli wa mambo ni kuwa nguvu anazokuwa nazo mtu wakati wa ujana wake zinaweza kufanya maajabu lakini kijana anahisi kwamba nguvu alizo nazo yaani hizi nguvu zake nyingi zilizorundikana ndani ya dhati yake na uwezo wake mkubwa alio nao, hautumiwi vile anavyotaka, hivyo hapo huhisi kwamba anapuuzwa na kudharauliwa. Tano, kwa mara ya kwanza mtu katika kipindi cha ujana wake huwa anaingia kwenye ulimwengu mkubwa na mpana ulimwengu ambao hajawahi kuuona na ndani ya ulimwengu huo mna vitu vingi asivyovijua. Mambo mengi humtokezea katika maisha yake na kumfanya aemewe, asijue cha kufanya. Hujihisi kwamba lazima apate mtu na kitu cha kumsaidia na kumuongoza na kutokana na kuwa mara nyingi baba na mama huwa wamebanwa na shughuli zao nyingine, huwa hawana wakati wa kushughulikia masuala ya kijana wao, matokeo yake ni kuwa kijana anashindwa kupata muongozo na msaada wa kimawazo na kifikra. Vituo na taasisi ambazo zimepewa jukumu la kufanya hivyo nazo ima haziko mahala panapotakiwa au hazina mipango mizuri ya kuufanikisha wajibu huo. Hivyo kijana anakosa msaada anaoutaka na kumfanya ajihisi hana pa kukimbilia.

Juu ya ukurasa

Kuamiliana Kihoja na Kijana

Kijana kwa kawaida hupenda sana kufafanuliwa mafundisho ya dini. Leo hii kijana anapenda kuifahamu dini yake kwa ushahidi na dalili zilizo wazi. Jambo hilo ni zuri na ni la mahala pake kabisa. Hilo ni jambo ambalo hata dini yenyewe ndivyo inavyowafundisha waumini wake. Qur’ani inatufunza kuwa, tuamini na tuamiliane na mafundisho ya Uislamu kwa kutafakari, kuzama ndani yake, kuangalia kwa mwangalio mpana na wa kina na tusikubali kuamini tu vivi hivi bila ya kuwa na ushahidi thabiti. Watu wanaohusika kama wataweza kuwafanya vijana wazame na kupiga mbizi katika kuangalia mambo kwa kina na kwa ushahidi kamili, basi watafanikiwa kuwafanya vijana wanamwabudu zaidi Mola wao na kushikamana vilivyo kivitendo na mafundisho ya dini yao.

Juu ya ukurasa

Hisia za Kijinsia

Suala la hisia za kijinsi ni miongoni mwa mambo yanayozishughulisha sana fikra za vijana na kwamba kadiri kijana anapopata mke au mume haraka ndivyo wasiwasi na akili yake inavyozidi kutulia. Mtazamo wangu kuhusiana na suala la kuoa na kuolewa vijana ni kwamba kama masuala ya mijamala na kupenda makuu katika masuala ya ndoa hayatakuwepo vijana wanaweza kila mmoja kuoa na kuolewa kiurahisi na kwa muda unaofaa lakini inasikitisha kuona kuwa suala la ndoa leo hii limefanywa ni kitu chenye gharama kubwa sana. Wakati wa ujana ndio wakati bora sana wa mtu kuoa na kuolewa. Lakini inasikitisha kuona kuwa watu wanafuata kibubusa utamaduni wa Magharibi kiasi kwamba baadhi ya familia zimebebeshwa fikra kuwa mtu anapotaka kuoa au kuolewa inabidi asubiri umri wake uwe mkubwa sana ndipo afunge ndoa, lakini katika Uislamu suala haliko hivyo. Katika Uislamu ni kwamba kadiri suala la kufunga ndoa linapokaribiana na miaka ya mwanzoni mwa ujana ni bora zaidi.

Juu ya ukurasa

Mashambulizi ya Kiutamaduni

Leo hii mashambulizi ya kiutamaduni yana uhusiano wa karibu sana na utumiaji wa teknolojia ya kisasa duniani. Leo hii kunatumika mamia ya vyombo na zana za kisasa za upashaji habari kwa ajili kuwamiminia propaganda hizi na zile vijana. Leo hii kunatumika anuwai kwa anuwai za vipindi vya televisheni, redio, kompyuta ni mithili ya vitu hivyo ili kujaribu kuziathiri fikra za vijana. Mfano mmoja ni kuwa wakati Wazungu walipotaka kuwapokonya Waislamu Andalusia waliamua kutekeleza ratiba na mipango ya muda mrefu. Wakati huo Wazayuni walikuwa hawajazuka bado, lakini maadui wa Uislamu na vyombo vya kisiasa vilivyokuwa dhidi ya Uislamu vilikuwa na nguvu. Maadui hao wa Uislamu waliona njia pekee ya kuwashinda Waislamu ni kueneza ufuska na vitendo vya ufisadi kati ya vijana wa Kiislamu. Waliofanya mashambulizi hayo walikuwa na misukumo mbali mbali ya Kikristo; kidini na kisiasa. Miongoni mwa mambo waliyofanya ni kurahisisha mno upatikanaji wa pombe miongoni mwa vijana wa Kiislamu! Aidha walihakikisha kuwa inakuwa rahisi sana kwa vijana wa Kiislamu kupata wasichana wa maadui hao wa Kiislamu wa kuweza kustarehe nao na kushibisha matamanio yao kinafsi na kwa njia hiyo wakawapotosha na kuwachafua vijana wa Kiislamu kwa tabia chafu za zinaa na mambo ya kiuasherati! Kwa kawaida ni kuwa kupita kwa muda na kubadilika kwa zama hakubadilishi njia kuu za ima kuharibu au kustawisha taifa. Leo hii pia maadui hao wa Kiislamu wanatumia mbinu hizo hizo kujaribu kuwapotosha vijana wa Kiislamu.

Juu ya ukurasa

Uvivu na Kupenda Wepesi na Starehe

Miongoni mwa maadui wakubwa zaidi wa mwanaadamu na ambaye anatoka ndani ya dhati ya mwanaadamu mwenyewe ni uvivu, kutopenda kufanya kazi, kupenda mambo mepesi mepesi na kutopenda kusumbuka. Inabidi watu wapambane vilivyo na adui huyu. Kama kijana atapambana na adui huyu na kufanikiwa kumshinda, wakati huo hataweza kushindwa na adui yeyote wa nje atakayejitokeza kumshambulia. Kama kijana ataweza kumshinda adui huyu, basi ataweza pia kumshinda adui ambaye anataka kupora suhula na utambulisho wa taifa zima. Lakini kama mtu atafanya uvivu na hataweza kumshinda adui huyu wa ndani ya nafsi yake, basi atashindwa kuingia kwenye medani ya ushindi wa adui wa nje. Hivyo adui mkuu wa mtu ni uvivu na kupenda wepesi na starehe. Mtu ambaye anajipinda katika kutafuta elimu, anayejipinda kufanya kazi, anayejipinda kufanya ibada, anayehakikisha anatekeleza wajibu wake mbali mbali wa kifamilia na kijamii kwa namna inayotakiwa, mtu ambaye haupi nafasi uvivu katika nafsi yake, kamwe hawezi kudai kwamba kama kutatokezea adui wa nje na kumshambulia, basi hataweza kumshinda.

Juu ya ukurasa

Kuvunjika Moyo

Iran imepata maendeleo makubwa sana katika sekta muhimu mno. Hizo ndizo harakati za Mapinduzi na huo ndio moyo wa Mapinduzi ya Kiislamu. Huko ndiko kujiamini ambako Mapinduzi ya Kiislamu inajipamba nako. Hiyo ndiyo anga na uwanja mpana ambao Mapinduzi ya Kiislamu yamewatunuku wananchi wa Iran ili waweze kuonesha vipaji vyao na huo ndio uwezo na fursa muhimu sana ambayo taifa la Iran imeipata kwa ajili ya kuweza kujipanga upya likiwa na matumaini makubwa ya ufanisi.

Kwa hakika fikra za baadhi ya watu za kuvunjika moyo na kudai kuwa “haiwezekani, hawaturuhusu, hakuna faida yoyote kufanya hili na lile” ni sumu hatari sana katika harakati yetu hii. Kuna wakati huko nyuma maadui wa Iran walikuja hapa nchini na wakaingiza sumu ya kuvunja watu moyo katika maji ya utamaduni wa taifa la Iran. Siku nyingine wakaja na kutwambia wazi wazi kwamba “nyinyi hamwezi kufanikiwa katika jambo lolote lile.” Wakati mimi nilipokuwa kijana, hayo yalikuwa ni miongoni mwa maneno yaliyokuwa yameenea sana hapa nchini. Tulikuwa tukiambiwa kwamba Muirani hawezi kutengeneza hata lulehang! Bila ya shaka mtakuwa mnajiuliza lulehang ni kitu gani tena. Lulehang ni neno la Kifarsi lenye maana ya aina ya mtungi tena mtungi wenyewe basi wa udongo. Huo ndio mtazamo waliokuwa nao wanasiasa na viongozi wa masuala ya Vyuo Vikuu wa wakati huo (wa kabla ya Mapinduzi ya Kiislamu) nchini Iran. Wanasiasa wengi wa wakati huo waliokuwa ni watu wa Vyuo Vikuu walikuwa wanasema wazi kwamba Muirani hana uwezo wa kufanya chochote! Lakini hapana, sisi tunasema, Muirani anaweza. Muirani anaweza kuvuuka mipaka ya elimu ambayo leo hii imepiga hatua kubwa sana. Muirani anaweza kuvuuka mipaka hiyo na kuingia kwenye mipaka mipya kabisa ya maendeleo ya kielimu.

Juu ya ukurasa

Madhara Yanayowakabili Vijana wa Kiislamu

Ulimwengu wa kibeberu na kiistikbari hautaki kumuona kijana wa Kiislamu anakuwa na azma na nia ya kweli ya kubakia msafi na mbali na madhambi. Hautaki kumuona vijana wa kiume na wa kike wa Kiislamu akiwa katika njia iliyonyooka ya umaanawi na ya kidini katika ulimwengu wa Kiislamu. Lakini kinachopaswa kufanywa na vijana wa Kiislamu ni kusimama kidete na kupambana na njama hizo za adui. Viongozi wa nchi za Kiislamu wanapaswa kujitolea kikamilifu kwa ajili ya kufanikisha jambo hilo kwa msaada wa vijana na kwa kulitegemea taifa hili. Viongozi hawapaswi kumuogopa mtu yeyote na inabidi wasikubali kutishwa na makelele ya adui. Ngome hii madhubuti ya taifa iko mikononi mwao hivyo inabidi wastafidi vilivyo na ngome hiyo ya vijana. Watu wa matabaka mbali mbali nchini hususan vijana, nao wajue thamani yao na wazifanye madhubuti nafsi zao.

Juu ya ukurasa

Kupambana na Madhambi

Maumbile salama ya kibinaadamu na ya kuheshimu amri za Mwenyezi Mungu, ni miongoni mwa hazina kubwa alizotunukiwa mwanaadamu na Muumba wake. Vijana wanapaswa kuyatumia vizuri maumbile hayo na waamue kikweli kweli kukabiliana na madhambi. Kuna baadhi ya watu wana fikra potofu kwamba mwanaadamu hawezi kupambana na madhambi, lakini hivyo si sahihi na uhakika wa mambo hauko hivyo. Inabidi mwanaadamu ailee nafsi yake na ajizoeshe kupambana na madhambi na bila ya shaka atafanikiwa. Katika kipindi cha ujana, wakati vijana wanapokuwa wameamua kutia nguvu azma na imani zao ili kukabiliana vilivyo na vishawishi vya kidunia, basi siku zote hufanikiwa. Tab’an Uislamu una njia nzuri za kumfanya mtu aweze kuizoesha na kuilea nafsi yake ikiwa ni pamoja na funga ambayo katika Uislamu ni faradhi iliyowekewa siku zake maalumu. Baadhi ya wakati mtu huona wazi wazi anaburuzwa upande wa kutenda madhambi. Lakini swali la kujiuliza hapa ni kuwa, je wakati mtu anapoona amekumbwa na wasiwasi wa kutenda madhambi, wakati huo huwa hana nguvu na uwezo wa kuamua asitende madhambi? Je hakuna njia yoyote ya kumwezesha asitumbukie kwenye shimo la madhambi? Ukweli wa mambo ni kwamba aghlabu ya wakati mwanaadamu huwa ni mwenyewe anayetaka kutenda madhambi na mara nyingi huwa na uwezo wa kujiepusha na madhambi, lakini hawaa na ushawishi wa nafsi humzuia kuchukua maamuzi yanayofaa. Baadhi ya wakati unaweza kumpata mtu amepitisha umri wake mzima akiwa ameshindwa kuamua kukabiliana na ushawishi wa kutenda mbadhambi, wakati mwingine mtu anakuwa mzee na anakosa nguvu za kweli za kuchukua maamuzi anayotaka, lakini kijana yeye anao uwezo na nguvu za kuamua. Kuna baadhi ya watu wanafikiri kuwa suala la kujiepusha na kutenda madhambi linawahusu vizee na vikongwe tu, wakati ambapo kama ambavyo nguvu za ujana wao huwa zimedhoofika, watu vizee huwa hupoteza pia nguvu zao za kiroho wanapofika uzeeni. Kwa kawaida kijana anakuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kuchukua maamuzi yanayofaa na huwa na nguvu kubwa zaidi za mapambano na istikama.

Juu ya ukurasa

Siri ya Maendeleo ya Vijana

Hazina Isiyoisha

Vijana na mabarobaro ambao wanajibidiisha kusoma Qur’an wajue kwamba wanajiwekea akiba kubwa itakayowasaidia kwenye umri wao wote katika upande wa kifikra na kuzingatia mambo. Jambo hilo lina thamani kubwa sana. Kuna uwezekano katika kipindi cha ujana wasiweze kujua kwa kina maana hasa ya aya wanazosoma za Qur’ani Tukufu, bali wakaweza kujua masuala ya juu juu tu yaliyomo kwenye mafundisho ya Kitabu hicho Kitukufu, lakini kadiri elimu yao itakavyokuwa inaongezeka ndivyo watakavyokuwa wanaweza kufaidika kwa upana mkubwa zaidi na aya za Qur’ani Tukufu ambazo walikuwa wameanza kujifunza na kuzihifadhi nyoyoni mwao tangu zamani. Ni neema kubwa sana kwa mtu kuwa na Qur’ani ndani ya kifua chake. Kuna tofauti kubwa baina ya mtu ambaye anapotaka kuelewa kitu fulani anaanza kuhangaika huku na huko kwenye faharasa za aya za Qur’ani ili aweze kujua maudhui anayoitafuta imezungumziwa wapi katika Qur’ani, na yule mtu ambaye aya za Qur’ani zimo kifuani mwake, anaziona wazi kwa macho yake na wakati wowote anapotaka kupata maarifa ya Kiislamu kuhusu jambo fulani anajua aende katika aya gani za Qur’an Tukufu. Ni neema kubwa sana mtu kuwa na mapenzi na uhusiano wa karibu na Qur’ani Tukufu wakati wa utotoni na wakati wa ubarobaro na kwenye kipindi chake cha ujana.

Juu ya ukurasa

Kutawakali kwa Mwenyezi Mungu

Vijana wanapaswa kutawakali kwa Mwenyezi Mungu. Waombe msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Imani zao za kidini wazitie nguvu katika nyoyo zao na watakapomudu kufanya hivyo watakuwa wamepata mafanikio makubwa iwe ni katika upande wa mafanikio ya kijana mweyewe, au katika mafanikio ya taifa zima. Vijana wanapaswa kuwa macho, wasiruhusu mambo yanayoharibu imani kuingia kama ukoma katika imani zao na kuangamiza imani hizo.

Suala la kutawakali na kumtegemea Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kwa ajili ya kuifanya batini ya mtu na moyo wake uweze kupata nguvu na kuwa imara. Kwa hakika kama tutazijenga batini zetu na kuzifanya kuwa imara, basi hakuna tatizo lolote la nje litakaloweza kutushinda. Inabidi kitu ambacho kimeifanya batini na nyoyo zetu ziwe imara na madhubuti, kiushinde pia upungufu wetu wa nje, wa kimwili na ule unaotokana na mazingira yaliyotuzunguka. Jambo hilo linawezekana kwa kutawakali kwa Mwenyezi Mungu na kuomba msaada wake.

Juu ya ukurasa

Kutia Nguvu Moyo wa Kujiamini

Vijana wanapaswa kujenga moyo wa kutafuta na kufanya kazi, moyo wa matumaini, moyo wa kujiamini na moyo wa kwamba “sisi tunaweza.” Miongoni mwa Waarabu kuna maneno yasemayo:

«ادّل دليلٍ على امكان شى‌ء وقوعه»

Hoja na dalili bora kabisa ya kuwezekana kitu, ni kutokea kwake.

Hivyo ushahidi bora kabisa wa kwamba kizazi cha vijana wa Kiirani kinaweza kufanya maajabu katika upande wa sayansi na teknolojia ni kuhakikisha wanafanya hivyo kivitendo na wanavuuka mipaka ya kielimu na kwenda mbali zaidi.

Juu ya ukurasa

Juhudi za Kielimu

Vijana hawapaswi kuzembea hata kidogo katika suala zima la kutafuta elimu na kuongeza uwezo wao wa maarifa. Kamwe wasitosheke na kiwango cha kazi walizofanya na daima wahisi kwamba ndio kwanza wako kwenye hatua ya awali. Vijana ni mithili ya wapanda milima, wanapaswa wapande hadi kileleni kabisa. Baadhi ya wakati mtu hutolewa jasho na hata vigingi na vizuizi vya mwanzoni kabisa mwa njia. Vijana hawapaswi kutosheka na mafanikio ya awali wanayopata bali wanapaswa wajue ndio kwanza wako chini ya mlima, inabidi waangalie kilele kiko wapi. Inawabidi vijana wafanye juhudi za ziada ili waweze kufika kileleni.

Juu ya ukurasa

Kutumia Vizuri Wakati

Vijana na mabarobaro wapendwa inawabidi watumie wakati kwa kiwango cha juu kabisa kadiri itakavyowawasiikia na itakavyoyumkinika. Tab’an jambo hilo nalo haliwezekani bila ya kuweko mipangilio mizuri. Hivyo wanapaswa kukaa chini na kupanga vizuri njia za kulifanikisha hilo kwa kutumia akili zao. Aidha wajue kuwa mipango haina kigezo kimoja kinachokusanya kila kitu na hatuwezi kusema kwamba kila mtu afuate kigezo fulani katika mipango yake. Kila mmoja anaweza kupangilia mambo yake kulingana na umri wake, kulingana na hali yake ya maisha ya kifamilia, kulingana na uwezo wake na kulingana na mji anaoishi na familia anayoishi nayo. Mipango inaweza kubadilika kulindana na hali halisi ya mambo ilivyo. Lakikni lililo muhimu ni kwamba kila mmoja anapaswa kuwa na mipangilio mizuri na atumie wakati wake kadiri itakavyowezekana kwa kujiwekea mipangilio makini na madhubuti yenye faida.

Juu ya ukurasa

Maswali ya Vijana na Majibu ya Ayatullah Khamenei

(Matini inayofuata ni ya maswali ya vijana kwa Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei na majibu yake kwa maswali ya vijana hao. Tab’an si maswali yote, bali ni baadhi tu ya maswali na majibu hayo).

Vigezo vyako katika kipindi cha ujana wako walikuwa ni watu gani?

Mtu ambaye aliniathiri sana katika kipindi cha ujana wangu - wa kwanza kabisa - alikuwa ni Marhum Nawwab Safawi. Wakati alipokuja Mashhad mimi nilikuwa na kama miaka kumi na mitano hivi. Kwa kweli aliniathiri sana kabisa na katika kipindi cha miezi michache tu baadaye walimuua shahidi kwa sura mbaya kabisa. Jambo hilo nalo liliniathiri sana. Baada ya hapo alikuwa ni Imam Khomeini ambaye aliathiri sana maisha yangu ya ujanani. Kabla ya mimi kuja Qum, na hata kabla ya kuingia katika mapambano yetu, nilikuwa tayari nimeshalisikia zamani jina la Imam Khomeini kabla ya hata sijaonana naye na tayari nilikuwa ninampenda na kumuheshimu sana. Sababu yake nayo ni kuwa, katika Hawza (Chuo Kikuu cha Kidini) ya Qum, vijana wengi walikuwa wakizipenda darsa zake, kwani darsa zake zilikuwa ni za kiujana na zilikuwa zinawavutia sana vijana. Tangu nilipofika Qum nilikuwa nikihudhuria darsa zake zote na sikukosa hata darsa moja hadi nilipoondoka Qum. Hivyo Imam Khomeini alinisaidia mno katika maisha yangu ya ujana. Tab’an baba yangu naye aliniathiri katika maisha yangu, mama yangu naye ameacha athari kubwa sana nzuri katika maisha yangu. Miongoni mwa watu walioniongoza na kunisaidia sana katika maisha yangu, ni mama yangu. Kwa kweli alikuwa ni Bimkubwa mwenye athari nzuri sana kwangu.

Juu ya ukurasa

Umepitisha vipi kipindi chako cha ujana?

Zama za ujana wetu zilitofautiana na zama hizi. Kwa kweli wakati huo hali ilikuwa mbaya sana. Mazingira aliyoishi kijana hayakuwa mazuri hata kidogo. Si kwangu mimi tu ambaye wakati huo nilikuwa mwanafunzi wa kidini, kwani mimi hata nilipokuwa mtoto mdogo katika shule ya msingi tayari nilikuwa ni mwanafunzi wa kidini, bali mazingira hayo mabaya yaliwakabili vijana wote. Watu walikuwa hawashughulishwi na masuala ya vijana. Vipaji vingi vya vijana vilikuwa vikipotea bure bila ya kutumiwa inavyotakiwa. Tulikuwa tunayashuhudia hayo mbele ya macho yetu. Mimi mwenyewe nilikuwa nikiyaona hayo katika mazingira ya uanafunzi wangu wa kidini. Wakati huo kuliwa na vijana wenye vipaji vya hali ya juu sana. Baada ya hapo pia na wakati nilipokuwa nikiingia katika mazingira ya nje ya uanafunzi wa kidini, nilipokuwa nikiingia katika mazingira ya Vyuo Vikuu na nilipokuwa nikiwasiliana na wanafunzi wa Vyuo Vikuu – na nilifanya hivyo kwa miaka mingi – nilikuwa nikiwaona na wao pia wanakabiliwa na hali hiyo hiyo. Kwa kweli niliona vijana waliokuwa na vipaji vikubwa na vizuri sana, lakini vipaji vyao vilidharauliwa. Ilikuweko idadi kubwa sana pia ya watu ambao pengine hawakuwa na vipaji vikubwa katika masomo waliyokuwa wanasoma lakini pengine walikuwa na vipaji vikubwa katika masuala mengine lakini hakuna mtu aliyejua au aliyefuatilia na kutaka kuvikuza vipaji hivyo.

Kabla ya Mapinduzi, kipindi changu chote cha ujana mara nyingi nilikuwa ninakitumia pamoja na vijana wenzangu. Baada ya kupata ushindi Mapinduzi ya Kiislamu, umri wangu ulikuwa ni kama miaka thelathini na tisa hivi. Kipindi changu chote cha kuanzia miaka kumi na saba, kumi na nane hadi wakati huo nilikipitisha pamoja na vijana iwe ni vijana wa Hawza na Chuo Kikuu cha Kidini au vijana waliokuweko nje ya Hawza. Hali niliyokuwa nikiishuhudia wakati huo ilikuwa ni kwamba, utawala wa kifalme wa Muhammad Reza Pahlavi ulikuwa unavuruga sana mambo kiasi kwamba vijana wengi walikuwa wanatumbukia kwenye mambo maovu na ya kujidunisha. Uovu huo haukumalizikia kwenye maadili na akhlaki tu, bali ulivuruga pia utambulisho na dhati ya vijana wenyewe na kuwafanya kuwa duni.

Tab’an mimi sikuweza kudai kuwa utawala huo ulipanga kwa makusudi mambo hayo ya kuwafanya vijana watumbukie kwenye maovu na masuala ya kujidunisha – pengine ilikuwa hivyo na pengine haikuwa hivyo – lakini kilicho na uhakika na ambacho naweza kukisema kwa yakini na bila ya kusita ni kwamba, utawala huo ulikuwa umevuruga mambo na ulikuwa ukiongoza nchi kwa namna ambayo, matunda yake yasingelikuwa kitu kingine ghairi ya kushuhudiwa hali hiyo yaani watu na hasa vijana kuwa mbali na masuala ya siasa na kuwa mbali na kufikiria kujiimarisha kimaisha.

Wakati huo matabaka yote ya watu wakiwemo vijana, walikuwa hawajishughulishi kabisa na masuala ya kisiasa. Mambo makubwa yaliyokuwa yakiwashughulisha vijana yalikuwa ni masuala ya kuhangaikia maisha yao ya kila siku tu. Baadhi yao walizongwa na masuala ya kutafuta mkate wao wa kila siku, walikuwa wakishughulishwa na kazi za sulubu ili waweze angalau kupata mkate wa kula. Tab’an kipato walichokipata hakikutumika tu katika masuala ya chakula, bali kilitumika pia katika mambo mengine ya pembeni.

Kama mtakuwa mumevisoma vitabu ambavyo viliandikwa katika kipindi changu cha ujana kuhusu Amerika ya Latini – kwa mfano vitabu kama vya Frantes Fanun (?) na waandishi wengine wa wakati huo – mtaona kuwa hali ya wakati huo ilikuwa ni kama nilivyosema. Kuhusu Iran hakuna mtu aliyekuwa akithubutu kuandika lakini kila mtu alikuwa huru kuandika masuala ya nchi kama za Kiafrika au kama za Chile na Mexico. Nilipokuwa nikisoma vitabu hivyo nilikuwa nikishuhudia na kuona kwamba hali iliyokuwa ikitawala Iran ilikuwa sawa sawa na hiyo. Yaani kijana alikuwa analazimika kufanya kazi nzito na za sulubu kiasi kikubwa sana lakini wakati alipokuwa akipata pesa zake basi ulikuwa unamuona anakwenda kuzitumia katika masuala ya kipuuzi, ya kujidunisha na ya kuharibu pesa. Vitu hivyo ndivyo nilivyokuwa nikivishuhudia kwenye vitabu hivyo na nilikuwa nikiona kwamba ndivyo hali ilivyokuwa kikamilifu nchini Iran. Kwa kweli hali ilikuwa mbaya sana. Mazingira aliyokuwa akiishi kijana wakati huo hayakuwa mazuri hata chembe. Tab’an kulikuwa na tofauti kati ya yale yaliyokuwemo kwenye nyoyo za vijana na mazingira waliyokuwa wakiishi ndani yake. Hali ilitofautiana kwani kimsingi vijana ni watu wanaopenda uchangamfu na hamasa na ni watu wa kupenda kuingia kwenye vitu vya kusisimua n.k.

Mimi mwenyewe nilikuwa kijana mwenye hamasa kubwa. Hali hiyo nilikuwa nayo hta kabla ya kuanza masuala ya Mapinduzi yaani hamasa na uchangamfu ulikuweko katika kazi zangu za kifasihi, kisanii na mfano wa hayo hadi baada ya kuanza harakati zangu za mapambano mwaka 1341 (1972) ambapo wakati huo nilikuwa na umri wa miaka 23. Tab’an kuanzia hapo niliingia katika hamasa za kimsingi za nchi yetu na katika mwaka wa 1342 nilikamatwa na kutiwa jela mara mbili, nilitiwa mbaroni, nilifungwa, nilisailiwa. Kama mnavyojua kwamba mambo hayo humtia hamasa maalumu mtu. Wakati mtu ulipokuwa unatoka kizuizini kwa mfano na kuona jinsi wimbi kubwa la watu wanavyothamini mapambano yenu sambamba na kuweko kiongozi makini kama Imam Khomeini (Mwenyezi Mungu Awe radhi naye) ambaye alikuwa akiongoza watu na kurekebisha mambo, fikra na njia mbali mbali za istikama na mapambano, basi hamasa zilikuwa zikikuongezeka maradufu. Hivyo ndivyo yalivyokuwa maisha kwa mtu kama mimi ambaye nilikuwa nikiishi katika mazingira ya mapambano na wakati wote nikifikiria vitu hivyo. Kwa kweli kipindi hicho kilikuwa kimejaa hamasa, tab’an hali haikuwa hivyo kwa vijana wote.

Wakati huo mimi na watu mfano wangu mimi ambao walikuwa wamezama katika masuala ya mapambano, hima yetu yote ilikuwa ni kwamba tujitahidi kadiri tulivyoweza ili kuwatoa vijana kutoka katika ushawishi wa kiutamaduni wa utawala wa kitaghuti. Kwa mfano mimi binafsi nilikuwa nikienda msikitini, nikitoa darsa ya tafsiri ya Qur’ani, nikitoa mawaidha baada ya sala na baadhi ya wakati nilikuwa nikienda mikoani kwa ajili ya tablighi na kutoa mawaidha. Nukta kuu niliyokuwa nikiizingatia mimi ilikuwa ni kuwatoa vijana kutoka katika ushawishi wa kiutamaduni wa utawala wa kitaghuti wa wakati huo. Wakati huo nilikuwa nikiviita vitu hivyo kwa jina la “wavu usioonekana.” Nilikuwa nikisema kwamba kuna wavu usioonekana ambao ulikuwa unajaribu kumtia mtegoni kila mtu! Ninataka kuhakikisha kuwa ninauchana kadiri nitakavyoweza ili niweze kuwatoa vijana kutoka katika wavu huo kadiri nitakavyoweza. Sifa ya kwanza iliyohitajika ili kufanikisha jambo hilo ilikuwa ni kushikamana na dini na pili ilikuwa ni kuwa na mielekeo na fikra za Imam Khomeini (MA) kwani mambo hayo yalikuwa ni ngao madhubuti kwa mtu aliyekusudia kufanikisha jambo hilo. Wakati huo hali ilikuwa hivyo. Kizazi cha vijana hao baadaye ndicho kilichokuja kuwa misingi mikuu ya Mapinduzi ya Kiislamu.

Juu ya ukurasa

Vitu gani vya kuburudisha vilikuwa vikijaza wakati wako katika kipindi cha ujana wako?

Ninasikitika kusema kwamba mimi sikuwa na vitu vingi vya kuniburudisha, kwani wakati huo hakukuwa na viburudisho vingi tofauti na hivi sasa. Tab’an bustani zilikuweko, lakini zilikuwa chache na kidogo mno. Kwa mfano huko Mashhad, kulikuwa na bustani moja tu ndani ya mji, na tena basi, mazingira yaliyokuwa yakitawala kwenye bustani hiyo yalikuwa mabaya sana. Mimi nilikuwa katika familia ambayo baba na mama ndani yake walikuwa ni watu walioshikamana na dini na haikuwa rahisi kwao kwenda katika maeneo yaliyokuwa na mazingira mabaya kama hayo kwani maeneo hayo hayakuwa mazuri na mara nyingi yalikuwa na mazingira machafu. Taasisi za wakati huo za dola nazo zilikuwa kwa namna fulani zikipenda kuona mazingira katika maeneo hayo ya uma yanachafuliwa kwa mambo ya ufuska na ufisadi. Awali ya mambo mimi nilikuwa nikikisia tu kwamba taasisi hizo zilipendelea hali hiyo iwepo lakini baadaye nilipata ushahidi na taarifa za uhakika zilizoonyesha kuwa, hisia zangu zilikuwa sawa yaani kulikuwa na mipangilio maalumu ya kuharibu mazingira ya mnaeneo hayo! Hivyo mimi nilikuwa siwezi kwenda kwenye maeneo kama hayo. Ndio maana nikasema sikuwa na vitu vingi vya kuburudisha kwani hali ilikuwa hivyo wakati huo na haikuwa kama ya leo hii.

Burudani niliyokuwa nayo katika mazingira ya uanafunzi wa kidini wakati wa ujana wangu ni kuwa pamoja na wanafunzi wenzangu. Tulikuwa tukienda madrasani kwetu madrasa ambayo ilikuwa inaitwa kwa jina la Nawwab na mazingira ya wanafunzi wa kidini yaliyokuwa yakitawala wakati huo yalikuwa ya kuvutia sana. Wanafunzi tulikuwa tukikusanyika pamoja na kuzungumza, kubadilishana mawazo na kupeana taarifa mbali mbali. Eneo la madrasa kwa wanafunzi wa kidini lilikuwa ni mfano wa klabu maalumu, kila tulipokuwa na wakati wa faragha tulikuwa tukienda huko na kukusanyika pamoja. Akthari ya hayo ni kwamba, huko Mashhad kuliwa na msikiti uliojulikana kwa jina la Goharshad ambao ulikuwa ni taasisi nzuri sana. Watu wa dini, wanafunzi wa kidini, masheikh na maulamaa walikuwa wakienda huko na wakijadiliana mambo mbali mbali ya kielimu. Baadhi ya mazungumzo yao yalikuwa ya kawaida na ya kirafiki. Hivyo ndivyo vilivyokuwa viburudisho vyangu.

Tab’an wakati huo mimi nilikuwa nikifanya pia mazoezi, hivi sasa pia ninaendelea kufanya mazoezi. Inasikitisha kuona kwamba vijana ni wavivu katika kufanya mazoezi na kwa kweli jambo hilo ni kosa kubwa. Wakati huo nilikuwa nikipanda milima na nilikuwa nikienda kwa miguu masafa marefu. Mimi na marafiki zangu tulikuwa tukienda mara nyingi katika milima hii na ile nje ya mji wa Mashhad na tulikuwa tukitembea kwa miguu kutoka kijiji kimoja hadi kingine hata nakumbuka baadhi ya wakati nilikuwa nikitembea kwa miguuu usiku na mchana.

Juu ya ukurasa

Kwa mtazamo wako, kijana wa Kiislamu anapaswa kuwa na sifa gani? Vipi kijana anaweza kupitisha kipindi cha maisha yake na akafanikiwa kufikia malengo yake?

Kama mtu anataka apate kitu chenye thamani basi anapaswa akubali kupata usumbufu na afanye juhudi za kutosha za kukifikia kitu hicho. Hilo ni jambo la lazima. Lakini angalieni kwa mtazamo wangu mimi, kuna sifa tatu muhimu zaidi kati ya sifa nyingine nyingi muhimu walizo nazo vijana. Iwapo sifa hizo tatu zitapatikana na kama zitaongozwa katika njia yake sahihi, basi nadhani hapo ndipo itakapowezekana kujibu vizuri swali lenu hili. Sifa hizo tatu muhiumu ni “nishati, matumaini na ubunifu.” Hizo ni sifa tatu kuu anazopaswa kuwa nazo kijana.

Tab’an katika Qur’ani kuna nukta ya kimsingi kabisa nayo ni taqwa. Wakati watu wanapotaka kuchora sura ya taqwa, akili zao huwapeleka kwenye sala, saumu, ibada nyinginezo, dhikri na dua. Naam, inawezekana yote hayo yakawa ni sehemu ya taqwa yaani ni vipengee katika taqwa lakini hatuwezi kusema kwamba vitu hivyo vyenyewe ndiyo taqwa. Maana ya taqwa ni kujichunga. Taqwa maana yake ni mtu kujua ni kitu gani anafanya na asichukue hatua wala asifanye harakati yoyote ila baada ya kuifikiria vizuri, dhati yake iikubali hatua hiyo na iamue kufanya kitu hicho. Mtu wa namna hiyo huwa ni mfano wa mtu aliyepanda farasi, akawa ametamakani vizuri juu ya mgongo wa farasi huyo, ujamu wa farasi uko mikononi mwake na anajua vyema anakotaka kwenda. Mtu ambaye hana taqwa, ni yule ambaye hadhibiti wala kuongoza harakati, maamuzi na mustakbali wake. Kama inavyosema khutba moja ndani ya Nahjul Balagha ambayo kiujumla maana yake inasema kwamba: Mtu ambaye wamempandisha kwa nguvu juu ya farasi mwitu haina maana kwamba amepanda mwenyewe. Hata kama atakuwa juu ya mgongo wa, hajui fani ya upandaji farasi. Lijamu imo mikononi mwake, lakini hajui amwendeshe vipi farasi. Hajui anakokwenda. Kokote atakakoelekea farasi na yeye atakwenda huko huko. Bila ya shaka yoyote mtu wa namna hiyo hawezi kuokoka na hawezi kufikia kwenye makusudio salama kwani farasi naye ni farasi mwitu, hapandiki na haongozeki.

Juu ya ukurasa

Kijana anaweza vipi kudhibiti hisia zake za kupenda mambo ya kusisimua na anaweza kufaidika nazo vipi hisia hizo?

Hamasa na mambo ya kusisimua yana mahala pake. Kuna baadhi ya vitu ndani yake huonekana kwa uwazi sana hali ya kusisimua. Mfano wake ni michezo – hasa hasa baadhi ya michezo kama vile mpira wa miguu – ni kitu chenye kuleta msisimko wa wazi. Hiyo ndiyo sifa ya mchezo wa mpira wa miguu na ni mchezo ambao unatofautiana na michezo mingine kama vile mpira wa vikapu na tennis. Hiyo inatokana na muundo wa mchezo wenyewe ambapo katika mpira wa miguu vitu kama upinzani, msisimko na vitu kama hivyo vinashuhudiwa sana na kwa uwazi zaidi. Kiujumla michezo ni kitu kinacholeta msisimko. Kazi za kisanii pia zina misukumo ya kusisimua lakini msisimko katika michezo hii mingine unaonekana kwa uwazi zaidi.

Masuala ya kusisimua hayahusiana na mambo hayo tu. Kama kijana ataweza kupata jambo analolipenda – popote alipo – anaweza kirahisi kupata msisimko anaoutaka. Kwa mfano wakati mimi nilipokuwa kijana na nikawa naona nimo katika mavazi ya mwanafunzi wa kidini, ni sawa mavazi yangu yaliniwekea mipaka maalumu, lakini wakati huo huo nilikuwa na vitu vya kufurahisha na kusisimua na niliweza kwa njia hiyo kushibisha hisia zangu hizo. Vipi? Ni kwamba mimi nilikuwa nikipenda sana tungo za kishairi. Tulikuwa na vikao maalumu vya kusoma mashairi na vikao vyetu hivyo vilinikusanya mimi na marafiki zangu wanne watano hivi ambao nao walipenda sana mashairi. Tulikuwa tukikaa masaa mawili, masaa matatu tukizungumza mambo mbali mbali kuhusiana na mashairi na tukisoma mashairi haya na yale. Hivyo kitu hicho kwa wale wapenzi wa mambo kama hayo huwapa motisha na msisimko kwa kiwango kile kile anachokipata mchezaji wa mpira wa miguu anapokuwa uwanjani au mpenzi wa mchezo huo wakati anapoangalia. Kwa hivyo medani na sehemu za kuweza kijana kushibisha na kukinaisha kwa njia sahihi hisia zake za kupenda vitu vya kuchangamsha na kusisimua ziko nyingi.

Mfano mwingine ni kuwa wakati mtu anapotaja jina la somo fulani, mtu mwingine anaweza kudhani kwamba somo hilo halina msisimko wowote. Ataona ni somo tu na hakuna msisimko wowote wa mtu kuweko darasani kusoma somo hilo. Lakini kama somo hilo hilo litafikiriwa kuwa kuna karakana iliyo na kila kitu pembeni mwa masomo ya darasani, ndani ya Chuo Kikuu au nje ya Chuo Kikuu – kama ambavyo leo hii imezoeleka kuwaona vijana wanaosomea masuala ya uhandisi wanakwenda kwenye karakana maalumu inayohusiana na fani yao – na kama katika hali hiyo, kijana wa namna hiyo atafanywa ahisi kuwa katika karakana hiyo kuna suhula ambazo zitamwezesha kutumia kipaji chake na ubunifu wake na kuutekeleza kivitendo ndani ya karakana hiyo na yeye akafanya hivyo, akapata shauku na hamu ya kwenda kwenye karakana hiyo. Kama hali itakuwa hivyo, bado mnadhani kwamba msisimko atakaokuwa nao kijana kama huyo utakuwa mdogo? Hapana, bali bila ya shaka yoyoe jambo hilo litampa msisimko mkubwa. Kazi za utafiti inabidi zitokane na mapenzi na shauku. Ninasema hivyo kwa sababu kama mtu atalazimishwa kuanya utafiti fulani bila ya yeye mwenyewe kupenda na kuwa na shauku na jambo hilo, kazi yake hiyo itakuwa kavu isiyo na faida yoyote.

Juu ya ukurasa

Unapowaona vijana unakuwa na hisia gani na neno la kwanza unalopenda kuwaambia ni kitu gani?

Wakati ninapokuwa na vijana na wakati ninapokuwa katika mazingira ya vijana hao, hisia zangu huwa sawa na hisia za mtu ambaye anavuta pumzi katika hewa ya alfajiri, huwa ninapata hisia mpya na nguvu mpya. Na kitu ambacho huwa kinanipitikia akilini na mara nyingi nimekuwa nikikifikiria akilini mwangu wakati ninapoonana na vijana ni kwamba je vijana hawa wanajua kwamba wao ni nyota zinazong’ara na zenye mwangaza wa kuvutia? Kama vijana watahisi kuwa na johari hiyo yenye thamani kubwa na ya kipekee, ninadhani kwamba Inshaallah wataweza pia kuitumia vizuri johari hiyo.

Juu ya ukurasa

Unawapa miongozo gani vijana ya kuweza kuitumia katika maamuzi yao mbali mbali ya kijamii na kisiasa?

Ninachopenda kuwaambia ni kwamba wasiogopeshwe sana na kuweko dhuku na hisia tofauti. Kuweko dhuku, mitazamo na hisia tofauti si jambo baya na pia hakuna matatizo yoyote kuweko kitu kama hicho. Kwa mfano kama vijana wawili watakuwa na hisia na mitazamo tofauti ya kisiasa; huyu akawa na itikadi hii na yule akawa na itikadi ile ya kisiasa; hilo si jambo baya. Jambo lililo baya na lenye madhara ni kuchukua hatua na kufanya mambo bila ya kuyafikiria wala kuyafanyia uchunguzi. Jambo baya ni kuchukua maamuzi ya pupa yasiyofanyiwa uchunguzi. Ninapenda kuwatahadharisha sana vijana juu ya jambo hilo. Hakuna ulazima kwamba madhali fulani ni kijana basi lazima achukue maamuzi ya haraka. Tab’an kijana hatakiwi kuwa msiri, mvivu na mwenye zohali katika mambo yake lakini hilo halina maana kwamba achukue maamuzi na afanye mambo kwa pupa na bila ya mipangilio maalumu. Kijana kama ambavyo hisia zake mara nyingine zinamfanya achukue hatua za pupa, ana uwezo mkubwa pia wa kufanya mambo kwa umakini wa hali ya juu na kwa fikra na utulivu mkubwa. Kama sifa hiyo - yaani sifa ya kuwa makini, kufanya mambo kwa kufikiria, kwa kuyachunguza na kwa kupigania haki – atakuwa nayo kijana - ambapo sifa zote hizo anaweza kuwa nazo kikamilifu kila kijana; baadhi yake kama kupenda mambo ya haki ambayo kimsingi ni sehemu na ni miongoni mwa sifa maalumu za vijana – basi tofauti za mitazamo baina ya vijana hao haziwezi kuwa kizuizi wala hazitapelekea kupotoka. Kwa ufupi ni kuwa madhara makubwa hayatatokea.

Suala la kuwakanusha wengine – yaani mtu kusema kuhusu masuala ya kijamii kwamba anachoamini yeye ndicho sahihi mia fil mia na hakuna kitu kingine sahihi isipokuwa chake yeye – jambo hilo si zuri hata kidogo. Tab’an katika baadhi ya misingi ya kiitikadi inabidi hali iwe hiyo yaani inabidi kuzifuatilia kwa kuzifanyika uchunguzi itikadi na kufikia hatua ya yakini, madhubuti na kusimama imara kwenye itikadi hiyo, lakini tunachokizungumzia hapa hakihusiana na itikadi za aina hiyo kwani linapofika suala la itikadi hizo inabidi msimamo uwe ni kwamba “itikadi hii ndiyo sahihi tu na yoyote isiyokuwa hii si sahihi” na hapo hakuna ubaya wowote kuwa na msimamo kama huo. Lakini katika masuala ya kijamii, katika kadhia za kisiasa na katika miamala mingine mbali mbali ya kijamii huwa si sahihi kuwa na misimamo kwamba “langu tu ndilo sahihi lisilo langu si sahihi.” Ninavyoona mimi ni kuwa inabidi mtu avumilie mitazamo na misimamo ya upande wa pili na afanye busara sana katika juhudi zake za kuthibitisha na kutia nguvu fikra zake. Ninavyoamini mimi ni kuwa kama hilo litatendeka basi hakuna matatizo yoyote yatakayotokea.

Juu ya ukurasa

Je, uko uwezekano wa kujazwa pengo lililopo baina ya Iran na nchi zilizoendelea?

Ninavyoamini mimi ni kuwa, majibu ya swali lenu hilo ni ndio. Inawezekana kabisa kujaza pengo lililopo. Nimekuwa nikiwaeleza mara nyingi wataalamu wetu kwamba Magharibi hivi sasa iko mbele sana kuliko sisi. Kama nchi yetu itaamua kufuata mbinu na njia ile ile iliyofuatwa na Magharibi ili kuwafikia walipo leo itabidi tupitishe karne nyingi sana za kuweza kufikia huko na hata hivyo pia hatutawafikia. Inabidi nchi zitafute njia za mkato za kuweza kufikia huko. Uvumbuzi wote huu wa kila leo tunaoushuhudia nchini mwetu ni miongoni mwa njia hizo za mkato. Lakini inabidi tujue kwamba Mashallah kuna njia nyingi mno za mkato za kuweza taifa kujiletea maendeleo ya kweli. Hiyo ndiyo dhati ya maumbile tuliyowekewa na Mwenyezi Mungu lakini sisi binaadamu bado hatujazigundua njia hizo. Kuna maelfu ya njia za mkato. Miongoni mwa njia hizo za mkato ni hii iliyofuatwa ya kufikia kwenye ustaarabu wa leo wa kiviwanda ambapo kila inapopigwa hatua moja basi hujitokeza hatua nyingine. Sasa kwa nini sisi tukate tamaa na tuvunjike moyo? Kuna wakati mwanaadamu hakuwa amevumbua umeme, yaani nguvu za umeme zilikuweko duniani, lakini mwanadaamu alikuwa hajazivumbua hata hivyo ghafla alizigundua zilipo na akaanza kuzitumia. Naam, aligundua nguvu za mvuke. Kabla ya hapo pia alikuwa moto haujui, lakini baadaye alikuja kuujua. Sasa kwa nini sisi tuvunjike moyo wakati ambapo bado kuna nafasi ya kugunduliwa kitu ambacho bado hakijagunduliwa duniani? Je hatuoni kwamba kila leo kunagunduliwa vitu vipya vipya? Inabidi tufanye juhudi za hali ya juu katika jambo hili ili tuweze kufika sehemu ambayo itaweza kutuzatiti haraka sana katika maendeleo ya kisanyansi na kielimu. Njia pekee ya kufanikisha jambo hilo ni kwa vijana wetu hususan vijana wasomi na wanaofanya utafiti mbali mbali wajipinde zaidi na kufanya kazi kubwa zaidi. Na kazi yoyote mnayotaka kuifanya inawezekana kuifanya katika kipindi cha ujana yaani katika nyanja zote tatu, uwanja wa elimu, uwanja wa kulea nafsi na uwanja wa michezo. Vijana wanapaswa kufanyia kazi vizuri nyanja zote hizo.

Juu ya ukurasa

 
< Nyuma   Mbele >

^