Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Baadhi ya Miongozo ya Walii Amri wa Waislamu Kuhusu Wananchi na Serikali ya Misri Chapa
31/01/2011

 Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, alisema mwaka jana wakati alipoonana na makundi ya wanamapambano wa Kipalestina kuhusiana na matukio ya eneo na suala zima la Palestika kwamba, ni jambo lisilo na shaka hata kidogo kuwa, Mashariki ya Kati mpya itaundika tu kwa kutegemea masuala ya uhakika yaliyokadiriwa na Mwenyezi Mungu na kwamba Mashariki ya Kati hiyo itakuwa ni Mashariki ya Kati ya Kiislamu.
Matukio yanayoendelea hivi sasa huko nchini Misri yamekuwa ni sababu tosha kwa mtandao huu wa Ayatullah Udhma Khamenei kukuandalieni makala maalumu ya kutupia jicho matukio yanayoendelea kushuhudiwa hivi sasa katika nchi za Kiislamu za eneo la Mashariki ya Kati.
(Sehemu ya kwanza ya makala hii maalumu itahusiana na miongozo ya Ayatullah Udhma Khamenei kuhusiana na wananchi na serikali ya Misri).

Wananchi wa Misri Hawatavumilia Usaliti wa Viongozi Wao
Marekani inafanya kosa. Kitendo cha Marekani cha kuzikusanya tawala za Kiarabu kwenye meza ya mazungumzo ya aibu kama haya kitawafanya wananchi wa nchi hizo zilizokusanyika kwenye mazungumzo hayo wazichukie tawala zao. Hivi (Wamarekani na vibaraka wao) wanadhani kwamba wananchi wa nchi za Kiarabu watakubali kuona viongozi wao wanakwenda kuiuza kwa wengine nchi ya taifa la Palestina? Mwenyezi Mungu apishie mbali mkataba kama huo usije ukatiwa saini lakini kama viongozi hao watatia saini mkataba huo, basi wajue kwamba ufa kati yao na wananchi utazidi kuwa mkubwa. Kitendo hicho kitawakasirisha mno wananchi wao. Wananchi wa Misri watakasirishwa sana na jambo hilo. Maskini Mmisri huyu! Amekwenda Marekani kama omba-omba eti kwenda kuishitaki Iran kwa Marekani! Kabla ya maskini huyu hajenda kushitaki kwa maskini mwenzake (Marekani), hiyo Marekani yenyewe nayo imejaa chuki dhidi ya Iran na inatamani ipate sehemu ya kwenda kushitaki!
Hivi kwa nini umekwenda huko kuishitaki Iran! Usiishitaki Iran, ushitaki Uislamu! Washtaki kwanza wananchi wako Waislamu! Kama bwana huyu ana hamu ya kushitaki, basi awashitaki kwanza wananchi wa Misri. Wananchi wa Misri ni Waislamu. Wananchi wa Misri wana historia kongwe katika Uislamu. Wananchi wa Misri wamefanya mambo mengi mazuri katika njia ya fikra mpya ya Kiislamu na mapambano ya Kiislamu. Taifa la Misri ni taifa lenye uchungu na dini yao. Ni jambo lililo wazi kwamba taifa hilo halitokubaliana na usaliti wa viongozi wao na bila ya shaka watapambana nao tu.
Mapambano ya wananchi wa Misri yanatuhusu vipi sisi? Sisi tunafurahi tunapoona Waislamu wa eneo lolote lile wameamka. Sisi tunafurahi tunapoona Waislamu wa eneo lolote lile wamesimama kupambana na maadui wa dini yao. Kila tunapoona Waislamu wanatesha na kukandamizwa, sisi tunachukia na kusikitika na tunahisi ni wajibu wetu kuwa pamoja na Waislamu wenzetu hao. Lakini sisi sio tutakaokwenda kwa mataifa hayo kama vile taifa la Misri na kuwapangia cha kufanya. Mataifa hayo yanajua wajibu wao. Wenyewe wana utambuzi wa kutosha kuhusiana na jukumu ambalo wanapaswa kulitekeleza na kwa kweli wanaonekana wazi kuwa wanaelewa majukumu yao. Wananchi wa Misri wameelewa vizuri majukumu yao. Vijana wa Misi wameelewa vyema kwamba ni wajibu wao kusimama kidete dhidi ya utawala ambao umesaliti malengo yao matukufu ya Kiislamu, malengo matukufu ya Palestina na hatima ya nchi za Kiislamu. Jukumu hilo ni la wananchi wenyewe wa Misri na si jukumu letu sisi. Tatizo la watu hawa (maadui wa Uislamu) ni kwamba hawaielewi nguvu na athari za dini tukufu ya Kiislamu.
(Sehemu ya hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyoitoa tarehe 28/4/1993 mbele ya wasimamiaji wa amali ya Hija wa nchini Iran).

Waislamu Walikuwa Wametengwa
Kuna tawala nyingi sana zimekuwa zikiingia na kutoka katika nchi za Afrika, Asia na Mashariki ya Kati huku Waislamu wakiendelea kutengwa na kuwekwa pembeni. Kwa mfano katika nchi kama ya Iraq, kuna wakati kulikuwa na utawala wa Kifalme. Utawala huo wa Kisultani na Kifalme uliondoka, ukaja utawala mwingine mahala pake. Utawala huo nao uliondoka na nafasi yake kuchukuliwa na tawala nyingine. Hivyo hivyo, hao wengine nao waliondoka na wakaja watawala wengine. Wakatoka viongozi hao wakaja watawala wengine mahala pao. Hali imeendelea hivyo hadi ukafika wakati wa utawala wa Kibaath. Katika kipindi chote hicho cha kubadilika tawala hizi na zile huko Iraq, watu wote walikuwa na nafasi katika tawala hizo isipokuwa Waislamu tu. Idadi ya wananchi karibu wote wa Iraq ni Waislamu, lakini nafasi yao haikupewa umuhimu wowote katika karne zote hizo za kubadilika tawala nchini humo! Au kwa mfano katika nchi kama ya Misri - tab'an nchini humo kuna kundi linalojulikana kwa jina la Ikhwanul Muslimin - lilipelekea kupatikana mabadiliko fulani na kupinduliwa utawala wa Kifalme. Baada ya kupinduliwa ufalme wa Misri nchi hiyo ilianza kutawaliwa na utawala wa Jamhuri na wa Kimapinduzi ukiongozwa na Rais Abdul Nasir. Baada ya kufariki dunia Abdul Nasir, akaja kiongozi mwengine, baada yake naye akaja kiongozi mwengine lakini katika kipindi chote hicho - tab'an hadi kabla ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran - Waislamu hawakupewa nafasi yoyote katika mabadiliko yote hayo. Ni kweli katika mapinduzi ya kwanza ya Misri, Waislamu walikuwa na nafasi, lakini waliwekwa pembeni mara baada ya kuundwa serikali mpya. Baadhi ya Waislamu hao walitiwa mbaroni na kutupwa jela, baadhi yao waliuliwa na baadhi yao wakatolewa kabisa katika uwanja wa siasa. Basi tunaweza kusema kwamba hata katika wakati huo pia, Waislamu hawakuwa na nafasi.
(Sehemu ya khutba za Kiongozi Muadhamu alizotoa kwenye sala ya Ijumaa ya tarehe 3 Ramadhani 1415 Hijria; Februari 3, 1995).

Kaulimbiu kama Iliyotolewa na Taifa la Iran
Nchini Misri hivi sasa wamejitokeza vijana, wamejitokeza wananchi na kuanza kutoa shaari na kaulimbiu za Kiislamu na ukizingatia mawasiliano ya kawaida yanayokuwepo baina ya watu wa kawaida, utaona Waislamu hao wa Misri hawana mawasiliano yoyote na wananchi wa Iran. Lakini nara na kaulimbiu za Wamisri hao ni sawa sawa na kaulimbiu zinazotolewa na wananchi wa Iran. Ajabu ni kuwa (maadui) wanamwambia Rais mwenye kashfa nyingi wa Misri kuwa watu hao wamechochewa na Iran! Sisi hatuna mawasiliano yoyote na Waislamu hao! Wamisri hao ni Waislamu na kaulimbiu zao za Qur'ani wanazitoa kwa sababu ni Waislamu. Ni wao wenyewe waliohisi wajibu wao wa kusimama na kupigania haki katika njia ya Mwenyezi Mungu (na kaulimbiu zao zinafanana na za wananchi wa Iran kwa sababu wote ni Waislamu). Shaari na nara zinazotolewa na wananchi wa Misri zinafanana kabisa na zile zilizokuwa zikitolewa na wananchi wa Iran wakati wa kupambana na Marekani, ubeberu na ukandamizaji wa kimataifa wakati wa utawala wa taghuti nchini, na kaulimbiu hizo dhidi ya ubeberu zinaendelea kutolewa hadi leo na wananchi wa Iran.
(Sehemu ya hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyoitoa tarehe 10/11/1992 mbele ya makamanda wa jeshi la Basiji kutoka kote nchini Iran).

Mabeberu Hawatofautishi Baina ya Shia na Suni
Mtu ambaye anaifanyia uadui asili ya Uislamu, uadui wake hauwezi kutofautisha baina ya Muislamu wa Kishia na Muislamu wa Kisuni. Tunashuhudia kwa macho yetu jinsi mabeberu wanavyowashinikiza wanamapinduzi wa Kiislamu wa Kisuni huko Palestina na Misri. Wanamapinduzi hao si Mashia wa Maimamu 12. Wote hao ni ndugu zetu Waislamu wa Kisuni. Lakini oneni jinsi mabeberu wanavyowashinikiza kupindukia. Mabeberu hawatofautishi, wanawaona Waislamu wote ni maadui wao. Lakini adui wa Uislamu na mataifa yote ya Kiislamu anafanya njama za kujipenyeza kwenye makundi na madhehebu mbali mbali za Kiislamu na kupanda mbegu ya chuki na uhasama katika safu za Waislamu. Adui anatumia fedha nyingi kufanikisha njama hiyo. Inabidi Waislamu tuwe macho!
(Sehemu ya hotuba ya Ayatullah Khamenei aliyoitoa mbele ya Masheikh tarehe 26 Disemba, 1989).

Kuteswa Makundi ya Waislamu nchini Misri
Makundi ya Kiislamu ambayo yamesimama kuulinda na kuutetea Uislamu, wanateswa, wananyanyaswa na kutupwa magerezani na viongozi wa nchi hizo. Madola ya kibeberu duniani nayo, yanawaunga mkono, yaani yanaziunga mkono tawala za nchi hizo. Hivi ndivyo ilivyo Misri leo hii. Hali ni hiyo hiyo pia katika nchi nyingine nyingi duniani.
(Sehemu ya hotuba ya Ayatullah Khamenei aliyoitoa tarehe 15 Novemba 1989 mbele ya kundi kubwa la majeruhiwa wa vita, familia za mashahidi na mateka wa vita).

Uungaji Mkono wa Marekani kwa Utawala Kibaraka wa Misri
Kizazi cha vijana kilichoelimika na chenye mwamko mkubwa nchini Misri kinaandamwa na kukandamizwa na utawala fasidi na usiostahiki kutawala nchini humo, huku serikali kibaraka na dhalili ya nchi hiyo kubwa (ya Kiislamu) ikipongezwa na kusaidiwa kifedha na kiusalama na Marekani.
(Sehemu ya ujumbe wa Ayatullah Udhma Khamenei kwa mahujaji wa Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu, tarehe 18/5/1993).

Wananchi wa Misri Wanawapenda Ahlul Bayt
Msikiti wa Raasul Husain wa nchini Misri - sehemu ambapo Wamisri wanaamini pamezikwa kichwa kitukufu cha Imam Husain AS - ni sehemu wanapokusanyika watu wenye mapenzi makubwa kwa Ahlul Bayt na watu wa nyumba ya Mtume Muhammad SAW huko nchini Misri. Wananchi wa Misri na watu wazuri. Sisi hapa hatuzungumzii utawala na serikali ya nchi hiyo. Tunachozungumzia sisi ni wananchi. Wananchi wa Misri wanawapenda Ahlul Bayt.
(Sehemu ya hotuba ya Ayatullah Udhma Khamenei aliyoitoa mbele ya maulamaa, wanafunzi wa dini na masheikh mbali mbali wakati wa kukaribia mwezi mtukufu wa Muharram tarehe 16 Juni, 1993).

 
< Nyuma   Mbele >

^