Skip to content

Habari

Habari
Hifadhi

Risala na Barua

Matini
Hifadhi

Kumbukumbu na Simulizi

Kabla ya Mapinduzi
Baada ya Mapinduzi

Sauti na Taswira

Picha
Sauti
Video
Dondoo za Miongozo ya Walii Amr wa Waislamu Kuhusu Vita vya Mabeberu dhidi ya Mwamko wa Kiislamu Chapa
02/02/2011

 Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, mwaka jana alionana na makundi ya wanamapambano wa Kipalestina na kuzungumza nao kuhusu masuala mbali mbali ya kieneo na kimataifa. Miongoni mwa miongozo aliyoitoa katika mazungumzo hayo ni kwamba, ni jambo lisilo na shaka kuwa kwa mujibu wa matukio ya uhakika yaliyokadiriwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mashariki ya Kati mpya itaundika katika eneo na kwamba Mashariki ya Kati hiyo itakuwa ni Mashariki ya Kati ya Kiislamu.
Kutokana na matukio yanayoendelea hivi sasa nchini Misri, tumeona ni vyema tukuandalieni makala maalumu wasomaji wa mtandao huu wa Ayatullah Udhma Sayydi Ali Khamenei ikiwa ni katika kutupia jicho matukio yanayotokea hivi sasa katika nchi za Kiislamu za Mashariki ya Kati na kuyapima na miongozo ya Walii Amr wa Waislamu.
Katika sehemu hii nyingine ya makala hii maalumu tumekuandalieni dondoo za miongozo ya Ayatullah Udhma Khamenei kuhusiana na vita vya mabeberu dhidi ya mwako wa Kiislamu.

Sifa za Kipekee za Qur'ani na Uislamu
Marekani inapinga Uislamu wa aina yoyote ile hata Uislamu usioko madarakani kama kiwango ya Uislamu kinachoshuhudiwa Saudi Arabia na Misri. Kwa mfano kama tutataka kufaridhisha kwamba pengine Marekani itafanikiwa kufikia malengo yake katika eneo hili jambo ambalo ni muhali, basi tayari tutakuwa tunajua wazi msimamo wao kuhusiana na nchi hizo utakuwa upi. Kuna wakati niliwahi kupewa ripoti kwamba afisa mmoja wa Marekani aliiambia moja ya wizara za nchi maarufu ya Kiislamu kuwa inabidi nchi yenu ipunguze masuala ya kidini na ya jihadi katika vitabu vya kusomeshea mashuleni. Alihoji kwa kusisitiza kwamba kwa nini mnaingiza vitu hivyo katika vitabu vyenu vya kusomeshea? Huo ndio ukweli wa mambo. Wamarekani wanapinga dhati ya Uislamu, wanapinga asili ya fikra ya Kiislamu fikra ambayo anayekuwa nayo humfanya asiogopeshwe na nguvu yoyote ya kidunia na kimaada na wala kutetereka. Hili ndilo linalowafanya Wamarekani wachukie na wahamaki. Na hii ndiyo sifa maalumu ya kipekee ya Qur'ani na Uislamu.
(Sehemu ya hotuba ya Ayatullah Udhma Khamenei aliyoitoa tarehe 18 Machi, 2002, mbele ya maafisa na wafanyakazi wa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu).

Nchi Vibaraka Vyao Nazo Ni Tatizo Kwao
Marekani haizipendi hata tawala wa Kifalme zinazotawala Mashariki ya Kati hivi sasa, kwani inahisi tawala hizo ni tatizo kwake. Tawala za nchi za Kiislamu na Kiarabu zinapaswa kulizingatia suala hilo. Marekani ina mipango maalumu kuhusiana na Misri kama ambavyo ina mpango amaalumu pia kuhusiana na Saudia. Ina mipango maalumu pia kuhusiana na Jordan na nchi nyingine za Ghuba ya Uajemi. Mipango ya Marekani haimalizikii kwa Lebanon, Syria na Iraq bali nchi nyingine za Kiarabu nazo nasikae tu na kuangalia kwa macho jinsi Marekani inavyomalizia hasira zake kwa nchi za Syria na Lebanon kama Washington inavyodhani. Nchi nyingine za Kiarabu zijue kwamba Marekani ikitoka Syria na Lebanon itazielekea nchi hizo za Kiarabu. Tab'an, Marekani bado ina safari ndefu sana ya kuweza kufikia malengo yake. Kundi la watu wanaotawala Marekani hivi sasa wanachukua misimamo yao kama walevi, hawajui wanachokifanya. Kwa kweli watu hawa wako mbali sana na ukweli wa mambo ulivyo duniani. Hata wachambuzi na weledi wakubwa wa masuala ya kisiasa nchini Marekani leo hii wanasema hivyo. Kurasa za Intaneti na magazeti ya Marekani nayo yanasema hivyo hivyo, yanasema kwamba kundi la watu walioko madarakani nchini Marekani wanaipeleka pabaya nchi hiyo, wanaipeleka Marekani kwenye kuporomoka na kusambaratika. Huo ndio ukweli wa mambo. Kuweko madarakani kundi la watu hao huko Marekani pengine kunaweza kuwa ni katika hasira za Mwenyezi Mungu; alaa kulli haal, viongozi wa Marekani wana mipango hiyo.
(Sehemu ya hotuba ya Ayatullah Udhma Khamenei aliyoitoa mbele ya wafanyakazi wa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran tarehe 30/10/2005).

Harakati za Kujipa Matumaini za Mabeberu
Wamarekani wanajua kuwa hawana lao katika ulimwengu wa Kiislamu. Wamarekani wanataka wawe na nafasi na wafanye mambo ambayo yatazuia mwamko wa Kiislamu usimalizikie kwenye harakati za kimapinduzi. Huo ndio mustakbali wa mataifa (ya Kiislamu) lakini Wamarekani wanabuni njia mbali mbali na kufanya harakati tofauti kujaribu kuzuia kutokea matunda ya mwamko wa Kiislamu. Ni hivi karibuni tu ambapo Wamarekani walikiri kuwa kama wasingeliivamia Iraq, basi utawala wa Saddam usingelidumu muda mrefu bali ungelitumbukia haraka mikononi mwa wananchi waumini na Waislamu wa Iraq na wakati huo Wamarekani wasingeliweza kufanya kitu kingine chochote. Kwa kweli wanaogopa. Hatua wanazochukua ni za pupa; zinatokana na woga walio nao kuhusiana na matokeo ya mwamko wa Kiislamu katika ulimwengu wa Kiislamu. Harakati zinazofanywa leo hii na Wamarekani katika eneo hazitokani na kuwa Wamarekani wana nguvu bali zinatokana na kuwa wameziona nguvu za kambi ya Kiislamu na udole wa harakati za Kiislamu na mbinde za mwamko wa Kiislamu.
(4/6/2005).

Kutojali na Kutoheshimu Utukufu wa Mwanaadamu.
Utawala wenu ni utawala uliojengeka juu ya chuki, dhulma na kutojali wala kuheshimu utukufu wa mwanaadamu. Kwa nini mumevamia Iraq? Kwa nini hamuheshimu heshima na matukufu ya wananchi wa Iraq? Hivi sasa wanaandaa mpango wa kubadilisha utawala, tab'an utawala ambao wanataka uwe unadhibitiwa na Wamarekani wenyewe. Wanasiasa na watu muhimu nchini Iraq wanapaswa wawe macho na wajue kuwa utawala wowote utakaoingia madarakani nchini Iraq na kugeuka kuwa utawala kibaraka wa Marekani basi wananchi wa Iraq hawatakuwa tayari kuuvumilia. Naam, wananchi wa Iraq hawawezi kukubali kuona kuwa baada ya kuondoka Saddam, utawala wa nchi hiyo unaingia mikononi mwa Marekani au vibaraka wake. Zoezi la kubadilisha utawala inabidi lihakikishe kwamba madaraka na utawala wa nchi hiyo unaingia mikononi mwa wananchi wa Iraq wenyewe, yaani kufanyike chaguzi, wananchi wenyewe wachague viongozi wanaowataka na isiwe ni kuja mtu na mpango unaopendwa na Marekani na kuwashinikiza wanasiasa na watu muhimu wa Iraq wautekeleze na kuwafanya wao nao wadhibitiwe na Marekani.
(16/5/2004).

 

 
< Nyuma   Mbele >

^