Miongozo ya Kiongozi Muadhamu kuhusu Uharamu wa Kuwavunjia Heshima Wake wa Mtume SAW
12/06/2016
Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema wakati alipoonana na maafisa wa kongamano la "Sadafe Kouthar" la kumuenzi Bibi Khadija SA kwamba: Kuwavunjia heshima wake wengine watoharifu wa Bwana Mtume SAW hakufai kabisa. Wake wa Mtume wanapaswa kuheshimiwa kwa hali yoyote ile. Mtu yeyote anayewavunjia heshima wake wa Mtume - yeyote awaye - ajue kuwa amemvunjia heshima Bwana Mtume mwenyewe. Ninayasema haya kwa yakini kabisa... angalieni namna Amirul Muminin (Imam Ali AS) alivyoamilia kwa heshima na Bibi Aisha, mtu ambaye alitoka kwa ajili ya kupigana naye vita, lakini (Imam Ali AS) aliamiliana naye kwa heshima yote ile. Bila ya shaka ni kwa sababu alikuwa ni mke wa Bwana Mtume, kwani kila mtu anajua vyema kwamba Amirul Muminin hakuwa na mchezo na mtu. Hivyo haifai kabisa kuwavunjia heshima wake wa Mtume SAW.