Kiongozi Muadhamu Aonana na Viongozi wa Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu
14/06/2016
Ayatollah Khamenei met with government officialsAyatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo jioni (Jumanne) ameonana na wakuu wa mihimili mitatu mikuu ya dola, yaani Serikali, Bunge na Mahakama pamoja na maafisa na wafanyakazi wengine wa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu, wakuu wa ngazi za juu wa taasisi mbali mbali nchini Iran pamoja na wanaharakati wa masuala ya kisiasa, kijamii na kiutamaduni na kusema kuwa, kuongezwa uwezo wa taifa katika masuala ya kimsingi hupelekea kupata kinga na kuwa imara taifa na nchi nzima kiujumla. Ameongeza kuwa: Kuweko mipango mizuri na kuainishwa vipaumbele katika utatuzi wa matatizo mawili ya kimsingi ya uzorotaji wa kasi ya ustawi wa kiuchumi na ukosefu wa kazi, kutaongeza kasi katika jitihada za ufanikishaji wa uchumi wa kimuqawama.
Mwanzoni mwa hotuba yake, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa nasaha kuhusiana na kutumiwa vizuri kadiri inavyowezekana anga ya kimaanawi ya mwezi mtukufu wa Ramadhani na ameashiria baadhi ya dua za mwezi huu mtukufu na kusema kuwa: Ndani ya baadhi ya dua za Ramadhani, kuna maombi ya kuokolewa na madhambi ambayo, kama viongozi watakumbwa na madhambi hayo - Mwenyezi Mungu apishie mbali - basi madhara yake yataikumba jamii nzima na nchi yote kiujumla.
Ayatullah Udhma Khamenei ameyataja baadhi ya madhambi hayo kuwa ni kutokuwa na malengo na msukumo wa jambo lolote, mghafala, kuwa na moyo mgumu, dharau na kutojali kitu pamoja na ghururi na kusema kuwa: Kama viongozi wa nchi hawatakuwa macho na wakashindwa kujilinda na madhambi hayo, hatua itakayofuatia ni ya hatari kubwa zaidi nayo ni kuwa dhaifu na kushindwa katika mambo mbali mbali, kukumbwa na unafiki na kukanusha neema za Mwenyezi Mungu.
Amesema, njia pekee ya kujiepusha na hatari hiyo na kujiweka mbali na madhambi hayo ni kujiimarisha kwa taqwa na kujichunga vilivyo na kuhakikisha hawakumbwi na matatizo hayo.
Baada ya hapo Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amegusia hali ilivyo hivi sasa nchini Iran na kusisitiza kwamba, nchi hivi sasa iko katika kipindi nyeti na maalumu na kuongeza kuwa: Miongoni mwa sifa maalumu za kipindi cha hivi sasa ambacho Iran imo ndani yake ni kwamba, tofauti na kipindi cha awali ya Mapinduzi, viongozi nchini sasa hivi wanazijua kikamilifu suhula na uwezo mkubwa wa nchi na wana welewa kamili na wa kila upande kuhusiana na uwezo mwingi na shula za kila aina zilizopo nchini.
Ayatullah Udhma Khamenei ameongeza kuwa: Sifa nyingine maalumu ambayo inaifanya hali ya nchini Iran kuwa nyeti hivi sasa ni kuweko uadui maalumu na ulio wazi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu na ambao ni mkubwa zaidi ya hitilafu za kawaida kati ya utawala moja na mwingine, na kati ya nchi na nchi nyingine.
Baada ya hapo amebainisha sababu kuu ya kuweko uadui huo maalumu kwa kusema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kitu kipya cha kipekee ambacho hakijawahi kutokea mfano wake duniani. Ameongeza kuwa: Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu umesimama juu ya msingi wa kifikra na kivitendo wa dini tukufu ya Kiislamu na umesimama imara kupambana na uistikbari, dhulma, ubaguzi na siasa za kibeberu na licha ya kuweko mashinikizo yote hayo; lakini nguvu na ushawishi wa Jamhuri ya Kiislamu katika eneo hili na duniani kwa ujumla unazidi kupanuka na kuwa mkubwa siku baada ya siku na kwamba hivi sasa Iran imekuwa ni dola kubwa linalochipua ambalo limeyaweka manufaa ya kidhalimu ya madola makubwa ya kiistikbari kwenye changamoto kubwa.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa: Kuna wajibu wa kuelewa na kutambua vyema njama na mipango ya adui na kuweka mipango kabambe ya kukabiliana na njama hizo kwa ajili ya kuilinda nchi ambapo mipango yetu ya utekelezaji na uendeshaji wa mambo nchini itakuwa na maana kama nayo itakuwa ndani ya fremu ya mpango huo mkuu.
Ayatullah Udhma Khamenei ameongeza kuwa: Mpango na njama za adui ni kuangamiza uwezo wa Jamhuri ya Kiislamu na kama adui atashindwa, basi anataka anagali aizuie Iran isiimarishe na kustawisha uwezo wake ilio nao hivi sasa.
Vile vile amesisitiza kuwa, njia pekee ya kuweza kukabiliana na njama za adui ni kutumia kwa njia sahihi na inayofaa uwezo mkubwa uliopo nchini na kuongeza nguvu zetu siku hadi siku. Baada ya hapo amebainisha uwezo na suhula kuu na kimsingi za Iran.
Kuwa na imani ya Kiislamu ni uwezo wa kwanza ambao Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameugusia katika hotuba yake hiyo na kufafanua kwa kusema: Upande wa pili unatumia suhula zake zote ikiwemo mawasiliano ya kompyuta na Intaneti ili kuteteresha imani ya dini ya Kiislamu kwa vijana na vizazi vijavyo vya Iran; hivyo, inabidi suala la kutia nguvu na kuimarisha imani hiyo ya Kiislamu katika jamii ikiwa ni moja ya nyuga za kulitia nguvu taifa, lazima lipewe umuhimu mkubwa.
Ayatullah Udhma Khamenei amelitaja suala la maendeleo ya kielimu kuwa ni ni nguvu ya pili na ya kimsingi iliyo nayo Iran hivi sasa na kusisitiza kuwa, upande wa pili unapinga vikali maendeleo ya kielimu ya Iran na unafanya njama mbali mbali ikiwa ni pamoja na hata kuwaua wanasayansi wa Iran kwa ajili ya kulizuia taifa hili lisiwe na maendeleo ya kielimu. Ameongeza kuwa: Maadui wanatumia hata mbinu za kiafiriti na kikhabithi ambazo zimepigwa marufu kama vile kutumia programu haribifu na virusi vya Intaneti kwa lengo la kulizuia taifa la Iran lisipate maendeleo ya kielimu na lau tungeliweza tungeliwaweka maadui hao mahali pabaya kwa jinai yao hiyo katika mahakama za kimataifa, amma kwa masikitiko ni kuwa jambo hilo halikufanyika.
Amekumbusha kuwa: Moja ya sababu kuu za mashinikizo ya maadui kwenye sekta ya teknolojia ya nyuklia ya Iran ni kupinga kwao maendeleo ya kielimu ya Iran na kwamba wenyewe maadui wanajua kuwa madai yao ya kwamba Iran ilikuwa na mpango wa kumiliki bomu la nyuklia ni uongo ulio wazi.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amezitaja nguvu na suhula nyingine za Iran kuwa ni uwezo wa kiuchumi na uwezo wa kujilinda na wa kuzuia kushambuliwa. Amesisitizia wajibu wa kuongezwa nguvu hizo na kusema: Uwezo na nguvu za kisiasa za kitaifa ambazo maana yake ni kuwepo umoja na mshikamano wa kitaifa, lazima zilindwe na ziheshimiwe, na licha ya kuwepo hitilafu na mitazamo tofauti ya kisiasa nchini - jambo ambalo halina tatizo lolot - lakini katika misingi ya harakati ya Jamhuri ya Kiislamu hakuna tofauti yoyote baina ya wananchi.
Ayatullah Udhma Khamenei ameongeza kuwa: Kwa taufiki na uwezo wa Mwenyezi Mungu, leo hii upo mshikamano na umoja huo wa kitaifa kwa ajili ya msingi mkuu wa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu na kiujumla ni kuwa wananchi wana mapenzi kwa Mapinduzi ya Kiislamu, kwa madhihirisho ya Mapinduzi ya Kiislamu, kwa kumbukumbu za Mapinduzi ya Kiislamu na kwa kwa jina na kumbukumbu ya Imam (Khomeini - quddisa sirruh).
Vile vile amesema, jamii yenye vijana wengi ya Iran, ni uwezo na nguvu nyingine kuu za taifa hili na kuongeza kuwa: Jamii ya vijana ni neema kubwa na muhimu na kwamba viongozi serikalini wanapaswa kuweka mipango sahihi ya kuhakikisha jamii ya vijana inaongezeka nchini.
Baada ya kutilia mkazo suala la kuongezwa aina sita za uwezo na nguvu za kimsingi za Iran katika kukabiliana na njama za maadui, Ayatullah Udhma Khamenei ametoa ufafanuzi kuhusiana na adui kwa kusema: Adui maana yake ni kanali ya kiistikbari na kibeberu ambayo inaongozwa na Marekani na pia kanali ya Kizayuni ambayo dhihirisho na mfano wake wa wazi ni utawala pandikizi wa Kizayuni (wa Israel).
Aidha amegusia kuwa, upande wa pili kamwe haufichi uadui wake dhidi ya Iran na kusema: Matamshi ya siku chache zilizopita ya Waziri wa Mambo ya Nje (wa Iran) katika kikao cha wazi cha Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (bunge la Iran) aliposema kuwa, dhati ya Marekani haijabadilika; ni matamshi sahihi kikamilifu, kwani dhati ya Marekani ya hivi sasa ndiyo ile ile ya zama za Regan na hakuna tofauti yoyote baina ya chama cha Democrat na chama cha Republican katika kuifanyia uadui Jamhuri ya Kiislamu na taifa la Iran.
Ayatullah Udhma Khamenei vile vile amegusia taswira moja ghalati na isiyo sahihi kuhusiana na Marekani na kusema: Kuna baadhi ya watu wanadhani kuwa, kuna siku sisi tunaweza kukubaliana na Marekani katika mambo yetu, na kuishi pamoja bila ya matatizo yoyote, lakini dhana hiyo si sahihi, bali ni ndoto.
Vile vile amesisitiza kuwa, kwa mtazamo wa kimantiki, kamwe Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haijawahi na haitawahi kupendwa na serikali ya Marekani na kusema: Vitendo vya Wamarekani daima vimekuwa vya kiafiriti, vya kikhabithi na ambavyo muda wote vimekuwa vya kiadui; hivyo kudhani kwamba masuala ya Iran na Marekani ni suutafahumu ambayo inaweza kutatuliwa kwa njia ya mazungumzo na kwa kutumia mbinu ya mapatano ya khamsini kwa khamsini, ni dhana ghalati na isiyo ya kweli.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aidha amesema: Ugomvi mkubwa wa Wamarekani ni uwepo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yenyewe na jambo hilo haliwezi kutatuliwa kwa mazungumzo na wala kwa kuwa na uhusiano kwani nguvu na uhuru utokanao na Uislamu, hauwezi kukubaliwa kamwe na madola ya kibeberu.
Ayatullah Udhma Khamenei amesisitiza kuwa, kwa mtazamo wa Marekani, mapatano maana yake ni kuachama na misimamo na misingi ya upande wa pili unaofikia mapatano na Marekani na kusema kuwa: Mwenendo wa kulegeza kamba na kuachana na misingi na misimamo ya upande huo unaofikia matano na Marekani huwa hauna mwisho kama ilivyojiri hivi sasa ambapo baada ya kumalizika kadhia ya nyuklia, Wamarekani wamezusha suala la makombora ya Iran, baada ya makombora litakuja suala la haki za binadamu, baada ya haki za binadamu itakuwa ni kadhia ya Baraza la Kulinda Katiba na baadaye suala la Fakihi Mtawala na mwisho itafikia kwenye Katiba ya Jamhuri ya Kiislamu na utawala wa Kiislamu nchini Iran; hivyo kudhani kuwa kuna siku Jamhuri ya Kiislamu inaweza kufikia makubaliano na Wamarekani na kumaliza uadui wao, ni dhana isiyo sahihi hata kidogo.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria pia dhana nyingine ghalati na potofu kwa kusema: Kuna baadhi ya watu wanatasawari kwamba, sababu ya uhasama na uadui wa Marekani kwa Iran, ni uchochezi na kupenda mivutano Jamhuri ya Kiislamu, wakati ambapo watu hao hao wamekuwepo tangu mwanzoni mwa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na wameuona wazi uadui wa Wamarekani kwa taifa la Iran kuanzia kutoa maneno mabaya, vikwazo, kutaka mambo yasiyokubalika hadi kuwapa hifadhi maadui wa taifa hili, na ni Wamarekani ndio waliojenga msingi wa uadui na mivutano na Jamhuri ya Kiislamu.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amelitaja suala la kinga na uwezo wa nchi kuwa ndiyo dawa ya kweli ya kupambana na kuushinda uadui wote huo wa mabeberu na kusisitiza kwamba: Kwa mujibu wa amri iliyo wazi ya Qur'ani Tukufu, tunapaswa kujizatiti kadiri tunavyoweza kwa nguvu za kiimani, kiuchumi, kiulinzi, kielimu, kisiasa na kijamii.
Vile vile amewataka viongozi wa taasisi zote nchini Iran kutekeleza vilivyo na kikamilifu majukumu yao katika mchakato mzima wa kuongeza uwezo wa kinga ya taifa na pia ametoa nasaha kwa maafisa wa wizara na taasisi zinazohusiana na kustawisha uwezo wa kielimu wa Iran kwamba wajiweke mbali na msambo ya pembeni na wazingatie wajibu na kazi zao za kimsingi.
Ayatullah Udhma Khamenei amesisitizia udharura wa kuungwa mkono na kusaidiwa vijana walioshikamana na dini na wanamapinduzi wakiwa ni moja na nguvu muhimu za nchi na kuongeza kuwa: Kama ambavyo nimekuwa nikifanya mara zote kwa uwazi kabisa ninasisitiza tena kusema kwamba ninawaunga mkono vijana waumini na wanamapinduzi na ninawapenda sana.
Kiongozi Mudhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameendelea na hotuba yake mbele ya viongozi na wakuu wa ngazi za juu wa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu kwa kutoa ukumbusho wa mambo kadhaa muhimu katika pande mbili za kiuchumi na makubaliano ya nyuklia yanayojulikana kwa jina maarufu la makubaliano ya JCPOA.
Amelitaja suala la kuzorota kasi ya ukuaji wa kiuchumi na ukosefu wa kwazi kuwa ni matatizo mawili makuu nchini na kusisitiza kuwa: Kabla ya matatizo hayo kuwa yanatokana na vikwazo; yanatokana kwanza na siasa na mipango ya serikai ya hivi sasa, serikali iliyopita na serikali za kabla yake.
Baada ya hapo, Ayatullah Udhma Khamenei amebainisha baadhi ya njia za kutatua matatizo hayo mawili kwa kusema kuwa ni kuvizingatia viwanda vidogo vidogo na vya wastani na kusema kuwa jambo hilo ni la dharura kwa ajili ya kutatua matatizo hayo. Ameongeza kuwa: Kuvifufua na kuvitia nguvu viwanda vya aina hiyo, ni katika mambo ya kimsingi ya uchumi wa kimuqawama na suala hilo linaweza kuisaidia kwa kiasi kikubwa harakati ya kiuchumi na kuandaa nafasi za kazi nchini.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu pia amesema, ni jambo muhimu sana kuainisha vipaumbele vya kufanyika kazi na kusisitiza kuwa: Ni jambo la kawaida kuona kwamba kila waziri anaona kuwa matatizo yake yeye ni muhimu zaidi na kufanya juhudi za kupata vyanzo vingi zaidi vya kutatua matatizo ya wizara yake, lakini serikali inapaswa kuainisha vipaumbele vya kweli na kuvipa umuhimu vipaumbele hivyo ili kuitia kasi harakati ya kiuchumi nchini.
Vile vile ameelezea matumaini yake kuwa matunda ya harakati za serikali yataonekana wazi katika suala zima la uchumi wa kimuqawama na kusema kuwa kuyasaidia mashirika ya kuzalisha elimu ni jambo ambalo linapaswa kupewa kipaumbele kikamilifu kwani lina mchango mkubwa katika kutatua matatizo mawili makuu yaliyopo, ya ukosefu wa ajira na kuzorota kasi ya ustawi wa kiuchumi.
Ayatullah Udhma Khamenei vile vile amelitaja suala la kuvutia na kuongeza inavyotakiwa uwekezaji na kuvutia vyanzo vya kigeni katika maeneo yanayohitajia uwekezaji wa aina hiyo nchini, kuwa ni jambo jingine muhimu na kusema: Inabidi kuwekwe vipaumbele pia katika suala hilo.
Kuzuia kuingia nchini Iran bidhaa ambazo mfano wake zinazalishwa pia nchini au bidhaa ambazo hazihitajiki Iran, kuboresha na kufanya vya kisasa vifaa vya viwandani, kuizingatia kikamilifu sekta ya kilimo, na kuzingatia na kuwekeza katika uzalishaji na kusafirisha nje bidhaa zinazotokana na mafuta na sio mafuta ghafi, ni nasaha nyingine zilizotolewa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa viongozi nchini.
Ameongeza kuwa: Kuongeza kiwango cha uzalishaji na usafirishaji nje mafuta ni miongoni mwa mahitaji ya nchi, lakini katika nchi ambayo ina akiba kubwa zaidi ya gesi na mafuta duniani, si jambo linalokubalika kuona inaagizia mafuta kutoka nje na kwamba viongozi nchini wanapaswa kulizingatia jambo hilo na kuweka mipango mizuri ya kulitatua.
Ayatullah Udhma Khamenei amekosoa mtazamo wa watu ambao wanadhani kuwa, hakuna vyanzo vya kutosha vya kufanikishia uchumi wa kimuqawama na kusema kuwa: Akiba za fedha za kigeni na fedha zilizohifadhiwa ndani ya hesabu za wananchi katika benki mbali mbali ni kubwa sana; sasa kwa kuongezwa usahilishaji na vivutio vya kisheria, vyanzo hivyo vinaweza kuelekezwa kwenye kutia kasi mchakato wa uchumi wa kimuqawama nchini.
Suala la makubaliano ya nyuklia baina ya Iran na kundi la 5+1 maarufu kwa jina la makubaliano ya JCPOA na kutolewa tathmini kuhusu kiwango cha kuheshimiwa makubaliano hayo na upande wa pili, ndiyo iliyokuwa sehemu ya mwisho ya hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu mbele ya viongozi na wafanyakazi wa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Ayatullah Udhma Khamenei amesema kuwa, mitazamo ya makundi yote mawili, lile linalounga mkono na lile linalopinga makubaliano ya JCPOA ina kuongeza chumvi ndani yake. Amesema: Watu wanaosifu makubaliano ya JCPOA na wale wanaoyakosoa na kuyapinga makubaliano hayo, wote wanaongeza chumvi katika kubainisha na kutoa mitazamo yao wakati ambapo makubaliano hayo yana nukta chanya na nzuri kama ambavyo pia yana nukta hasi na dhaifu.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa: Mambo mazuri yaliyomo kwenye makubaliano ya JCPOA ni yale mambo ambayo yaliivutia Jamhuri ya Kiislamu kufanya mazungumzo ya nyuklia, tab'an hadi kuna mambo mengi mazuri hayakupatikana.
Vile vile amegusia mambo mabaya na mapungufu yaliyomo kwenye makubaliano ya nyuklia ya JCPOA kwa kusema: Mambo hayo ni yale ambayo sisi muda wote tulikuwa na wasiwasi nayo na mara zote tulikuwa tukisema kwa kusisitiza kuwa, upande wa pili wa mazungumzo hayo, ni upande usioheshimu ahadi zake; ni upande ambao dhati yake ni mbaya; ni upande ambao hausiti hata kidogo kwenda kinyume na ahadi zake.
Ameongeza kuwa: Ndani ya makubaliano ya JCPOA kuna nyufa na tundu ambazo lau kama zingelizibwa, basi mapungufu na kasoro za makubaliano hayo zingelikuwa chache au zingeliondoka kabisa.
Ayatullah Udhma Khamenei ametoa ufafanuzi kuhusu juhudi kubwa na nzito zilizofanywa na timu ya mazungumzo ya nyuklia ya Iran na kusisitiza kuwa: Mambo ambayo tunayasema hapa kuhusiana na makubaliano ya JCPOA hayahusiani hata kidogo na ndugu zetu azizi walioendesha mazungumzo hayo, bali maneno yetu haya yanaulenga upande wa pili wa makubaliano hayo.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amegusia kona zilizojaa utata za hati ya makubaliano ya JCPOA ambazo zinaandaa uwanja wa kutumiwa vibaya makubaliano hayo na upande wa pili na kusisitiza kuwa: Jamhuri ya Kiislamu haitakuwa ya kwanza kuvunja au kwenda kinyume na makubaliano hayo, kwani kutekeleza ahadi ni amri iliyomo ndani ya Qur'ani Tukufu, lakini kama vitisho vinavyotolewa na wagombea urais wa Marekani wanaojigamba kuwa watayachana makubaliano hayo iwapo wataingia madarakani - kama vitisho hivyo - vitatekelezwa kivitendo, basi wajue kuwa Jamhuri ya Kiislamu itayachoma moto kabisa makubaliano hayo ambapo kufanya hivyo nako ni katika kutekeleza amri ya Qur'ani Tukufu kuhusu majibu wanayopasa kupewa watu wanaokengeuka na kwenda kinyume na ahadi zao.
Ayatullah Udhma Khamenei ameendelea na hotuba yake kwa kutoa ufafanuzi kuhusu ushahidi wa kivitendo na wa wazi wa namna Marekani inavyokwepa kutekeleza ahadi zake na kusema kuwa: Jukumu la upande wa pili wa mazungumzo hayo lilikuwa ni kuondoa vikwazo, lakini haukutekeleza jukumu hilo, yaani kuna baadhi ya vikwazo vimeondolewa kwa namna fulani lakini kivitendo ni kuwa vikwazo havijaondolewa.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa: Wamarekani wameviacha kama vilivyo vikwazo vyote vikuu na vya daraja la kwanza jambo ambalo linaathiri moja kwa moja suala la uondoaji wa vikwazo vya daraja la pili.
Ayatullah Udhma Khamenei amesisitiza kuwa: Wahusika wote wana wajibu wa kuzingatia na kuwa makini katika jambo hilo wala wasirudie maneno kuwa vikwazo vimeondolewa.
Amegusia pia namna matatizo ya miamala na benki za nje yalivyoshindwa kutatuliwa na kusema: Viongozi wa serikali ya Marekani utawasikia wanasema kwa maneno kuwa hakuna kizuizi chochote katika miamala ya benki za Iran na benki za nje, lakini kivitendo wameweka mazingira ambayo benki za nje hazithubutu kuwa na miamala ya kibenki na Iran.
Ayatullah Udhma Khamenei amesema kuwa matamshi ya hivi karibuni ya kiongozi mmoja wa Marekani aliyesema kuwa, sisi hatuwezi kuichia Iran ifanye mambo yake kwa uhuru, ni mfano wa wazi wa vitendo vya kindumilakuwili vya Wamarekani na kuongeza kuwa: Marekani imefanya kosa na uhalifu huo mkubwa wa kuweka vizuizi katika miamala ya kibenki baina ya Iran na benki za kigeni na mtu yeyote yule hapaswi kutafuta njia za kuhalalisha vitendo hivyo vya Wamarekani.
Bima za meli za mafuta za Iran ni maudhui nyingine ambayo Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameitolea mfano wa uvunjaji na ukengeukaji wa ahadi unaofanywa na Marekani na kusema: Tab'an Wamarekani wamekubali kuwepo kiwango kidogo cha bima hiyo lakini miundo mikuu ya bima haimo ndani ya kiwango kilichokubaliwa na Wamarekani kwani ndani ya miundo hiyo mikubwa, Wamarekani ni wananchi huko, na wanakwamisha ufanikishaji wa jambo hilo.
Vile vile amesema, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetekeleza kikamilifu ahadi zake katika makubaliano hayo na kuongeza kuwa: Sisi tumekuwa mara zote tukitoa malipo kabla ya wakati wake kufika na mara kwa mara tumekuwa tukionesha kivitendo namna tunavyoheshimu makubaliano hayo, na tumesimamisha urutubishaji wa urani kwa asilimia 20 na hata taasisi zetu za nyuklia za Fardo na Arak nazo tumezisimamisha, lakini bado upande wa pili unataka mambo mapya.
Ayatullah Udhma Khamenei amemlenga moja kwa moja katika maneno yake mkuu wa Taasisi ya Nishati ya Nyuklia ya Iran akimwambia kwa kusisitiza kwamba: Kamwe usikubaliane na matakwa ya upande wa pili kuhusiana na kaboni zinazotumika katika utengenezaji wa mashinepewa kama ambavyo usikubaliane kabisa pia na suala la mizani ya kilo 3000 ya mada za nyuklia.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria pia fedha za Iran zilizozuiwa nje ya nchi na kusema: Leo hii kupata malipo yatokanayo na uuzaji mafuta ya nchi yetu limekuwa ni jambo zito na lenye gharama kubwa, na hata fedha tulizo nazo katika benki za nchi nyingine hadi hivi sasa haijarejeshewa Jamhuri ya Kiislamu kwani fedha hizo zimo katika sarafu ya dola na kuzihamisha kumepigwa marufuku kutokana na uadui na kukosa mwamana Marekani.
Akiendelea na hotuba yake, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, teknolojia ya nyuklia ni teknolojia ya kiistratijia na inabidi idumu na istawishwe bila ya dosari yoyote.
Amegusia pia taathira za teknolojia ya nyuklia katika suala zima la kuiwekea kinga Iran na kuongeza usalama wa nchi na kusisitiza kuwa: Uwezo wa teknolojia hiyo, nguvu kazi yake ya watu wenye uwezo mzuri na uwezekano kuirejesha katika hali yake ya kabla ni mambo ambayo inabidi yachungwe na yalindwe.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa: Kwa bahati nzuri uwezo wa kurejea katika hali yake ya kabla umelindwa na sisi tunaweza wakati wowote tutakapohisi kuna haja ya kufanya hivyo, kufikisha kizazi kipya cha mashinepewa zetu kwenye idadi ya mashinepewa laki moja, katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu, hivyo upande wa pili usijidanganye kudhani kuwa tumefungika mikono.
Ayatullah Udhma Khamenei amesisitiza kuwa, kuna wajibu wa kukabiliana vilivyo na vizuizi na ubinyaji wa aina yoyote ile unaofanywa na Marekani na amewalenga moja kwa moja viongozi nchini akiwaambia kwa kusisitiza kuwa: Haki si ya kuomba, haki ni ya kuchukuliwa hususan wakati haki hiyo inapokuwa katika mdomo wa mnyama hatari kama Marekani.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameelezea kufurahishwa kwake na matamshi ya Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri Kiislamu na Waziri wa Mambo ya Nje (wa Iran) yaliyohusiana na kupambana vilivyo na ukwamishaji wa mambo unaofanywa na Marekani na kusisitiza kwamba: Tunapaswa kuhifadhi na kulinda uwezo wetu wa kila namna katika kukabiliana na uhasama na vitendo vya kiuadui vya upande wa pili.
Vile vile amesema kuwa, kufanikiwa Iran kujirutubishia urani kwa asilimia 20 na uwezo wake wa kutengeneza mashinepewa za kisasa ndizo sababu kuu zilizoifanya Marekani ikubali kutoa baadhi ya ahadi na kusisitiza kuwa: Lau kama si uwezo wa kisayansi na kiteknolojia wa Iran, bila ya shaka yoyote Wamarekani wasingelikubaliana na hata hali hii ndogo ya hivi sasa, hivyo kuna wajibu wa kuongezwa uwezo wetu huo wa kisayansi na kiteknolojia kwa kadiri inavyowezekana.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema katika nukta yake ya mwisho kuhusiana na kadhia ya nyuklia katika hotuba aliyoitoa mbele ya viongozi na wafanyakazi wa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu kwamba: Tunachotarajia kutoka katika timu ya kusimamia utekelezaji wa makubaliano ya JCPOA ni kufanya mambo yake kwa umakini na kuzidi kuwa macho na kwamba katika hatua yoyote ile ambayo upande wa pili utafanya kinyume na inavyotakiwa au kuwa na nia ya kufanya usaliti, timu hiyo isimame imara na kulinda vilivyo manufaa ya taifa.
Kabla ya hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Hujjatul Islam Walmuslimin Hassan Rouhani, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa hotuba fupi na kusema kuwa, mwezi mtukufu wa Ramadhani ni mwezi wa rehemu ya Mwenyezi Mungu na huku akigusia hali iliyo nayo Iran hivi sasa tangu ilipoingia madarakani serikali yake amesema: Serikali ya kumi na moja ya Jamhuri ya Kiislamu inalipa umuhimu suala la kudhibiti mfumuko wa bei na kupanda maisha na imeweza kudhibiti mfumuko huo kutoka asilimia 40.1 mwaka 1392 (mwaka wa Kiirani wa Hijria Shamsia sawa na mwaka 2013 Milaadia) na kuufikisha asilimia 11.9 mwishoni mwa mwaka 1394 na kwamba katika mwezi ujao, kiwango hicho cha mfumuko wa bei kitakuwa cha rakamu na nambari moja.
Rais Rouhani amesema pia kuwa, mafanikio mengine ya serikali yake ni kudhibiti soko la fedha za kigeni, kuleta ustawi wa kiuchumi na kutatutua kikanikifu suala la uzorotaji wa kasi ya ukuaji wa kiuchumi.
Katika sehemu nyingine ya hotuba yake Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amegusia hatua zilizochukuliwa na Serikali katika sekta ya kilimo na kusema kuwa: Kuanzia mwaka 1392 hadi 1394 (2013 hadi 2015), uzalishaji wa bidhaa za kilimo umepanda nchini Iran kutoka tani milioni 97 hadi tani milioni 112.
Rais Rouhani ameongeza kuwa: Katika upande wa kuweka akiba na bidhaa za chakula cha kiistratijia kama vile ngano na mchele, akiba hiyo imeongezeka mara tatu mwaka 2015 ikilinganishwa na mwaka 2013 na kwamba imetabiriwa kuwa, uzalishaji wa ngano nchini Iran mwaka huu utapanda hadi tani milioni 10, kiwango ambacho takriban ni sawa na mahitaji yote ya Iran kwa bidhaa hiyo.
Ameashiria pia maendeleo yaliyopatikana katika sekta ya mafuta na kusema: Vitengo vya 12, 15, 16 na 17 vya eneo la Pars Kusini vyote vimefunguliwa na vitengo vingine vitatu hadi vinne vinatarajiwa kufunguliwa na kuanza kufanya kazi ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuwa: Uzalishaji wa gesi ya Iran katika kipindi hicho umeongezeka kwa mitakubiki milioni 150 kwa mwaka.
Vile vile amegusia ongezeko la ujpenzi wa njia za reli nchini na kusema: Kwa kuongezeka kilomita 475 za njia za reli huku kukiwa na mipango wa kuongeza ujenzi wa kilomita 700 za njia hizo, kutaleta mabadiliko makubwa katika upande wa usafiri wa reli na usafirishaji wa bidhaa nchini.
Rais Rouhani amesema pia kuwa, kuna mabadiliko makubwa na mazuri katika upande wa biashara na kusisitiza kuwa: Mwaka jana, na baada ya kupita miaka 60, kwa mara ya kwanza usafirishaji nje bidhaa za Iran zisizo za mafuta umepindukiwa kiwango cha uingizaji wa bidhaa hizo nchini.
Vile vile amesema: Kwa wastani, katika kipindi cha miaka minane iliyopita, kiwango cha biashara nchini kilikuwa ni dola "-25 bilioni" lakini kwa mara ya kwanza kiwango hicho hivi sasa kimekuwa katika rakamu chanya.
Rais Rouhani vile vile amegusia mazungumzo ya nyuklia na kusema: Tumeweza kuthibitisha haki ya Iran ya kuwa na teknolojia ya nyuklia kupitia mazungumzo hayo kama ambavyo tumeweza pia kuyafuta maazimio ya kidhalimu yaliyokuwa yamewekwa dhidi yetu.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aidha amesema, hatua ya mwanzo ya baada ya kuondolewa vikwazo ni kupata fursa ya kuingia katika soko zuri la kuuza bidhaa na kusema, hivi sasa tumekaribia kufikia katika hali tuliyokuwa nayo kabla ya kuwekwa vikwazo katika uwanja huo.
Rais Rouhani amebainisha kuwa, uzalishaji wa gesi asilia nao umepanda kutoka mapipa laki tatu na 70 elfu na kufikia mapipa laki tatu na 90 kwa siku katika miezi ya hivi karibuni na kuongeza kuwa: Usafirishaji wa mafuta ghafi ya Iran leo hii umeongezeka kwa mapipa milioni mbili na kwamba uzalishaji wa mafuta nao umepanda kutoka mapipa milioni 2.7 hadi mapipa milioni 3.8 kwa siku.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa: Hivi sasa Iran inahitajia mno kuwa na umoja na mshikamano kwa ajili ya kufikia malengo yake.
Amesema, suala muhimu zaidi lililoko mbele ya Iran hivi sasa ni suala la nafasi za ajira na huku akibainisha kwamba, moja ya fakhari za serikali ya kumi na moja ya Jamhuri ya Kiislamu ni kwamba katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita imefanikiwa kuzalisha nafasi milioni moja na laki tatu na 40 elfu mpya za kazi na kuongeza kuwa: Kwa mujibu wa kituo kikuu cha takwimu nchini Iran, hivi sasa kuna wafanyakazi zaidi ya milioni 22 nchini.
Amesema, moja ya matatizo ya kufikia kwenye ustawi unaotakiwa wa kiuchumi, ni uchache wa mahitaji na kuongeza kuwa: Bila ya kuweko soko jipya hatuwezi kufikia kwenye ustawi unaotakiwa wa kiuchumi, hivyo tuna wajibu wa kutafuta soko jipya la ndani na nje pamoja na kuvutia uwekezaji wa kigeni.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria pia matamshi ya hivi karibuni ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kuhusiana na ukosefu wa ajira kwa vijana na kusema kuwa: Ukosefu huo wa ajira unaisononesha sana Serikali hasa inapoona kuwa, vijana wasomi wa Kiirani, hawana kazi.
Rais Hassan Rouhani amebainisha pia kuwa, tangu mwaka jana, kamati ya kusimamia uchumi wa kimuqawama imeundwa kwa amri ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kusema kuwa: Hadi hivi sasa kamati hiyo imeshafanya vikao 19 tofauti na kuandaa mipango 110 kama kipaumbele kikuu cha kazi zake.
Aidha Rais Rouhani amesema, hatupaswi kufifiliza na kupunguza imani ya wananchi na ya jamii na kuongeza kuwa: Kama katika sehemu na pembe fulani wametokezea baadhi ya watu na kuchukkua mishahara mikubwa zaidi, jambo hilo tusiligeuze kuwa kadhia ya taifa zima, na kwamba Serikali imefungua vizuri masikio yake kusikiliza ukosoaji kutoka upande wowote ule.