Risala Kufuatia Ajali ya Kuhuzunisha na Iliyopelekea Kufariki Dunia Askari kadhaa Vijana
25/06/2016
Ayatulla Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, ametoa ujumbe maalumu wa mkono wa pole kufuatia ajali mbaya ya barabarani iliyopelekea askari kadhaa vijana kupoteza maisha yao. Amesisitiza kuwa, wahusika wote wa ajali hiyo wanapaswa kufuatiliwa kisheria kwa kadiri inavyotakiwa.
Matini kamili ya ujumbe huo ni kama ifuatavyo:

Bismillahir Rahmanir Rahim
Nimeipokea kwa masikitiko makubwa habari ya ajali mbaya ya barabarani iliyopelekea kupoteza maisha askari wetu vijana waliokuwa kazini kulihudumia taifa. Ninatoa mkono pole kwa udhati wa moyo wangu kwa familia zilizokumbwa na msiba huo nikimuomba Mwenyezi Mungu azimiminie rehema Zake familia hizo katika mikesha na siku hizi zilizojaa baraka. Maafisa wa kijeshi na wasio wa kijeshi wana wajibu wa kufuatilia inavyotakiwa suala hilo na kuchukua hatua zinazostahiki kuchukuliwa. Roho za vijana wetu azizi hazipaswi kuingizwa kwenye hatari za namna hii.
Sayyid Ali Khamenei
5 Tir 1395
(Juni 25, 2016)