Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Aonana na Rais na Maafisa wa Serikali
24/08/2016
Ayatollah Khamenei met with Prayer Leaders from across Tehran provinceAyatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, leo asubuhi (Jumatano) ameonana na Rais Hassan Rouhani na maafisa wa serikali yake na sambamba na kuishukuru Serikali ya 11 ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, maadhimisho ya Wiki ya Serikali ni fursa nzuri inayobidi itumike vizuri kwa ajili ya kutoa ripoti kwa wananchi kuhusu kazi nzuri zilizofanywa na serikali hadi sasa.
Aidha amezungumzia nukta nyingine kadhaa muhimu ndani ya vifungu saba tofauti na kuzungumzia masuala ya uchumi wa kimuqawama, siasa za mambo ya nje, sayansi na teknolojia, suala la usalama, utamaduni, mpango wa sita wa maendeleo na suala la Intaneti vikiwa ni vipaumbele vikuu vya Iran na muongozo wa Serikali ya 11 katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa: Ripoti iliyotolewa na Serikali kuhusu kazi ilizozifanya katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita ni nzuri sana, lakini inabidi mambo hayo waeleweshwe vizuri wananchi kwani rasilimali kuu ya Jamhuri ya Kiislamu ni imani ya wananchi.
Aidha ameitumia fursa hiyo kuwaenzi mashahidi Muhammad Ali Rajai, Rais wa zamani na Muhammad Javad Bahonar, Waziri Mkuu wa zamani wa Iran na kusema kuwa, inasikitisha kuona kwamba kuna baadhi ya watu wanafanya kampeni za kusahaulisha jinai zilizofanywa na wanafiki waliouwaua kidhulma maelfu ya wananchi wa Iran wakiwemo viongozi hao muhimu wa Iran ambao walikuwa ni vigezo vizuri vya ikhlasi na uchapaji kazi. Hata hivyo amesema, njama hizo zitashindwa tu, kama zilivyoshindwa huko nyuma.
Ayatullah Udhma Khamenei amesema, suala la utamaduni ni katika vipaumbele muhimu mno kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusisitiza kuwa, suala la utamaduni linajumuisha mambo mengi kama vile sanaa, fasihi, mtindo wa maisha pamoja na mienendo na maadili ya watu katika jamii na kwamba vyuo vikuu vya masuala ya kiutamaduni vina jukumu kubwa na zito katika masuala yote hayo.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu pia amesema, utatuzi wa matatizo yaliyopo ya kiuchumi ni kutekeleza kwa kina na kwa njia sahihi siasa za uchumi wa muqawama, na kuzielekeza benki na kiwango kikubwa cha matumizi ya fedha taslimu, upande wa uzalishaji wa bidhaa za ndani, kutoa vihamasishaji vya kusafirisha nje bidhaa, na kuipa umuhimu sekta ya viwanda vya vijijini na mashambani. Amesema, hizo ni katika hatua za kimsingi za kutekeleza kivitendo siasa za uchumi wa muqawama.
Ayatullah Udhma Ali Khamenei aidha amesema, siasa za mambo ya nje ni moja ya vipaumbele vya serikali ya Iran katika muda wote huu na kuongeza kuwa: Mabara ya Asia, Afrika na Amerika ya Latini inabidi yapewe nafasi yanayostahiki katika siasa za mambo ya nje za Iran.
Amma kuhusiana na suala la usalama, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, kutokana na juhudi kubwa za vikosi vya ulinzi na usalama, Iran imeweza kuwa na ngao na kinga madhubuti ya kiusalama licha ya kuzungukwa na nchi zilizojaa machafuko na ukosefu wa amani katika eneo hili...